Kukunja mahindi kunaweza kuwa na faida nyingi kwa mavuno yako ukiifanya vizuri kwa usahihi.
Kukunja mahindi ni njia maarufu katika Amerika ya kati na ina faida tofauti. Mbinu hii huzuia maji mengi kuingia katika ncha ya gunzi. Kwa hivyo, mmea hukauka vizuri bila ya kuoza na magonjwa mengi. Pia, punje hazishambuliwi na ndege mara nyingi.
Hivyo, mahindi yataacha kukua na hayatapokea maji, chakula na virutubisho kutoka kwenye mizizi tena. Hakikisha kupata wakati wema wa kukunja mahindi.
Wakati sahihi wa kukunja
Maadamu mahindi ni kijani, jua kwamba bado yanakua. Lakini wakati mmea huu unapoanza kuwa wa manjano na unaonekana kama majani hapo basi ni mzima kabisa. Dondosha mbegu kadha kwenye gunzi na uangalie nche ya mbegu kama ni nyeusi. Ikiwa imegeuka nyeusi, basi unaweza kuikunja. Jua kwamba tukikunja mahindi mapema, mbegu hupunguza uzito na ubora.
Mahindi yanayokua polepole huhitaji muda zaidi mpaka yaweze kukunjwa. Ikiwa una mahindi yanayokua haraka, unaweza pia kuongeza mazao ya msimu wa pili kwenye shamba lako kama vile maharagwe au ufuta.