Kilimo cha uhifadhi, ni muhimu kwa kulinda na kuboresha udongo.
Wakulima wengi hupata changamoto za kiangazi, magugu mengi, na upotezaji wa rutuba ya udongo. Kulima hufanya udongo uwe kavu na kushambuliwa na wadudu na magonjwa, au mmonyoko wa udongo. Ikiwa unataka kulinda udongo wako, ni muhimu kuulima mara kidogo unavyowezekana. Funika udongo na mimea, na pia fanya mzunguko wa mazao. Kufuata hatua hizi huitwa kilimo cha uhifadhi.
Kuboresha Udongo
Hatua ya kwanza ni kuua magugu kwa kutumia dawa badili ya kulima. Baadaye, subiri hadi wiiki moja ili kuhahikisha magugu yote yamekufa ndio uendele na kuchimba mashimo.
Unaweza kufunga zana mbili za kulima kwa fahali au punda. Piga mitaro ukitumia mafahali. . Jembe ya kufungua udongo (ripper) ambayo ina michongo ya chuma ni nzuri kutumia ikiwa udongo hujaganda.
Ikiwa udongo umeganda, unafaa kutumia zana ya subsoiler ili kuchimba urefu wa kutosha ardhini. Kawida, tumia zana hii kwa mwaka moja hadi miwili ya kwanza.
Zana zote mbili hufungua mtaro bila kugeuza udongo. Baada ya kufungua udongo, weka mbolea ya samadi ili kuboresha udongo . Hatua hii ni muhimu hasa katika mwaka wa kwanza wa kilimo cha uhifadhi.
Tumia zana ya kupanda kwa sababu hupanda mbegu pamoja na mbolea. Awali, tumia mbolea ya samadi wakati ukianza kilimo cha uhifadhi. Hakikisha kwamba unapanda mara bada ya kuchimba. Ni humimu kwamba kupanda kunafaa kuanza kabla mvua ya kwanza. Ukipanda katika wakati wa kiangazi, bomba za zana ya kupanda zinaweza kuziba. Hakikisha kwamba unapanda katika mistari
Baada ya miaka minne, haufai kulima wala kunyunyiza dawa ya magugu tena. Matandiko yatafunika magugu . Dawa za magugu huhatarisha mazingira na maisha ya watu. Kama hauna matandiko ya kutosha, endelea kutumia dawa za magugu.
Badilisha mazao ili kudhibiti wadudu na magonjwa. Mazao tofauti hutenda tofauti kwa wadudu na magonjwa.
Katika mwaka wa pili hadi wa nne, utashuhudia mafanikio katika shamba lako.