Magugu ni shida kwa wakulima, kwa sababu hunyonya na kupunguza maji na virutubisho vya mimea ya mpunga. Kwa hivyo, ni muhimu kujua jinsi ya kudhibiti magugu.
Kutofautiana na mpunga, magugu mengi hufa palipo na maji. Mbegu za magugu hupatikana kwenye mchanga, na huenea kwa upepo na maji. Mbegu zingine za magugu huchanganywa na mbegu za mpunga. Magugu huwa na uharibifu mkubwa wakati wa wiki sita(6) za kwanza baada ya upanzi.
Kudhibiti magugu
Kulima huua na kuzika mbegu za magugu, hali kadhalika haziwezi kuota. Magugu mengi huangamizwa ikiwa shamba limefurikwa au kuloweshwa kwa wiki mbili. Kwa hivyo unafaa kulima na kufurika mara mbili kabla ya kupanda.
Safisha mifereji ya maji na kando za shamba kutokana na magugu. Hakikishwa kwamba unapanda mbegu safi ambazo hazina magugu. Kwa kutumia mbegu bora, unapata mimea yenye nguvu na inaweza kustahimili magugu. Aina za mbegu ambazo hukua mapema hustahimili magugu vizuri.
Ukipandikiza au kuatika miche ya wiki mbili, unampa mmea wako nguvu dhidi ya magugu. Kama huna wakati wa kuatika,basi panda mbegu zilizooteshwa moja kwa moja katika shamba. Weka mbegu katika maji na uondoe zile zinazoelea. Hakikisha kutumia mbegu zenye afya ambazo hazina magugu. Ziache mbegu usiku kucha katika maji, hadi asubuhi ufuatao ndio uzitoe. Kisha, acha ziote kwa siku mbili.
Magugu zaidi hukua ikiwa kuna nafasi kubwa katikati ya mimea ya mpunga. Katika maeneo ya nyanda za chini, mbegu zinaweza kupandwa kwa umbali wa 15 cm hadi 20cm kati yazo. Kupalilia ni rahisi sana ukipanda mimea ya mpunga kwenye mistari.
Unapopanda moja kwa moja, basi unafaa kupalilia baada ya wiki tatu kwa mara ya kwanza. Wiki mbili hadi tatu baadaye, unaweza kupalilia kwa mara ya pili. Kwa mpunga uliopandikizwa, unahitaji kupalilia mara moja tu wakati mimea inapoanza kuota (ambapo mmea hutoa matawi manne). Hapo ndipo wakati mzuri wa kuongeza nitrojeni(mbolea). Dawa za kuua wadudu pia zinaweza kutumika, lakini sio zote zinafaa kudhibiti magugu. Shamba linafaa kuwa safi kutokana na magugu, ili kusitorutubisha magugu.