Ardhi iko hatarini kwa uharibifu, kwa hivyo wakulima wanafaa kujua kwamba maisha yao hutegemea kudumisha rutuba ya udongo. Wanyama na miti husaidia kuzuia uharibifu wa ardhi.
Samadi hupendelea kwa wakulima, kwa hivyo wakulima wasio na wanyama wana uhusiano mwema na wafugaji. Wafugaji wanafaidika na mabaki ya mazao ya wakulima, na vile vile huwapa wakulima samadi kwa malipo. Samadi ni muhimu kwa mtama na uzalishaji wa chakula.
Ushirikiano wa jamii
Jamii huanzisha vyama ili kusaidia katika kuboresha uhusiano wa kutegemeana kati ya wafugaji na wakulima. Baada ya msimu wa mvua, wafugaji hukubaliana na wakulima kuacha samadi shambani na kukubali wanyama kukaa hapo kwa siku chache hadi wiki.
Wakati miti inakua zaidi ya matawi 9, wakulima wanaruhusiwa kukata hadi matawi 3 wakifuata sheria za upandaji wa miti. Mikakati kati ya wakulima na wafugaji hufanywa kwa msingi wa familia. Miti hunasa nitrojeni kutoka hewani, hutoa kivuli na pia ni chanzo cha lishe la mifugo.
Samadi huvunjwa vunjwa kwa vipande vidogo ili kuboresha rutuba ya udongo. Mabaki ya mimea na lishe kutoka kenye miti hutengenezwa kupitia kutafunwa na wanyama na kuwa maziwa kwa wafugaji.