Maji ya mvua yanayotiririka yanaweza kubadilishwa kuwa muhimu yakivunwa. Hii inaweza kufanywa kupitia mashimo ya upandaji ya Zai, ambayo hutumiwa kupokea mtiririko wa maji juu ya ardhi.
Mashimo ya Zai huchimbwa kwa mkono na jembe: yakiwa na kipenyo cha 25cm, kina cha 20cm, na muachano wa 90cm kwa kila mwelekeo. Udongo uliochimbuliwa huwekwa chini ya mteremko wa shimo.
Mbolea ozo huwekwa kwa usahihi kwenye mashimo ya zai kabla ya kupanda mtama au mawele. Kwa hivyo mvua inaponyesha, unyevu na virutubisho hujikusanyia haswa vinapohitajika.
Faida za mashimo ya Zai
Mbolea oza na mbolea ya kikaboni inayowekwa kwenye mashimo ya zai hutumika vizuri. Nafaka, kunde na mabaki ya mazao hutoa chakula kwa mifugo. Mashimo huongezwa na mistari ya mawe ambayo huwezesha udongo uliomomonyoka kujikusanyia katika Zai.
Zai hupanua mavuno na husaidia kuboresha hali ya ukame na jangwa kwa kupokea na kuhifadhi mtiririko wa maji. Miti pia hupandwa kwenye mashimo ya zai kama vile mishita ambayo yanaweza kutumika kama matandazo
Kuandaa mashimo ya Zai
Mashimo hutengenezwa kwa kutumia jembe liyoboreshwa ambayo huvutwa na farasi ili kufungua mistari. Reki iliyoboreshwa huvutwa kwa pembemraba ili kuonyesha mahali pa kutengeneza shimo la zai. Kisha mashimo huchimbwa, na mbolea huwekwa ndani. Njia hii hupunguza pembejeo ya wafanyikazi.
Nchi kama vile Burkina Faso na Niger hutumia njia ya mashimo ya zai.