Kupima uotaji wa mbegu ni muhimu sana kwa sababu kunawasaidia wakulima kubaini uwezo wa mbegu, kujua kiwango cha mbegu cha kupanda, na kuokoa muda. Kwa hiyo uliza kila mara kuhusu kiwango cha uotaji wa mbegu wakati utakapozinunua.
Kipimo cha uotaji lazima kifanyike wiki mbili kabla ya kupanda mbegu. Ikiwa asilimia 85% ya mbegu zilizopandwa zimeoota, hizo ni mbegu nzuri sana. Ikiwa asilimia 84% ya mbegu zilizopandwa zimeoota, hizo pia ni nzuri, lakini chini ya 60%, hizo si mbegu nzuri za kupanda.
Hatua
Tayarisha shamba kwa kukata na kufyeka vichaka.
Pima eneo la futi 7 kwa 7, kwa utunzaji na usimamizi rahisi wa shamba.
Ondoa magugu kwenye eneo lililopimwa, tandaza eneo hilo ili kuhifadhi maji udongoni ambayo husaidia mbegu kuota.
Lima na ulainishe udongo ili kuwezesha mbegu kuota kwa urahisi.
Mwagilia eneo kila baada ya siku 2, na linda shamba ili kuhakikisha matokeo bora.
Pata matokeo siku 6–7 wakati mbegu zimeota.
Hesabu mbegu zilizoota, na ufasiri matokeo. Ikiwa 85% ya mbegu zimeota, panda mbegu 2 kwa kila shimo. Ikiwa 84%, panda mbegu 3 kwa kila shimo, na ikiwa chini ya 60% mbegu hizo ni mbaya na usizipanda.