Ugonjwa wa kiwele ni hatari kwa mifugo na unasababishwa zaidi na hali duni ya usafi, na huenea kutoka titi moja hadi jingine, kwa hivyo kagua uwepo wa ugonjwa kabla ya kukamua.
Ugonjwa wa kiwele huonyesha dalili kadhaa katika wanyama ambazo baadhi yazo ni; mnyama hukataa kukamuliwa, matiti huumia, nyufa kwenye kiwele, uvimbe wa kiwele, ulaji mdogo wa malisho, maziwa ya maji, kuganda kwa maziwa, na damu kwenye maziwa. Upimaji wa ugonjwa wa kiwele hufanyika kwa kutoa matone machache ya maziwa kutoka kwa kila titi, na kuwekwa kwa kipimaji.
Kuzuia uvimbe wa kiwele
Daima safisha banda la ng‘ombe kwa kuondoa chakula kilichomwagika na samadi mara kwa mara.
Kamulia ng‘ombe katika sehemu safi iliyombali na sehemu ya kulala.
Pia osha mikono kwa maji safi yenye sabuni kabla ya kukamua ili kuepuka kuenea kwa vijidudu kutoka kwa wagonjwa hadi kwa wanyama wenye afya bora.
Zaidi ya hayo safisha kiwele na matiti ya ng‘ombe na uyakaushe kwa kitambaa safi.
Usikamue kiholela ili kuepuka michubuko kwenye matiti ambayo inaweza kuingiza vijidudu.
Ongeza kinga ya wanyama dhidi ya ugonjwa kwa kuwalisha wanyama vizuri.
Kamua maziwa yote kutoka kwenye kiwele ili kuepuka vijidudu kukua kwenye maziwa iliyobaki.
Walishe ng‘ombe mara tu baada ya kukamuliwa ili kuepusha mnyama kulala chini na hivyo kusababisha mgusano wa matiti na ardhi amabao huingiza vijidudu.
Hatimaye, lisha ng‘ombe kwa majani ya mitishamba ili kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa.
Matibabu ya uvimbe wa kiwele
Kwanza, kanda kiwele na matiti ukitumia maji ya majani ya mpera yaliyochemshwa.
Pili, weka mafuta yaliyochanganywa na poda ya manjano na chumvi kwenye matiti ili kuua viini.
Ongeza dondoo ya majani ya mwarobaini, maji na mafuta kwenye matiti mara mbili kwa siku ili kuua viini.