»vipandikizi vya Mihogo – Video ya Mafunzo«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=Sca4nzHXrH8

Muda: 

00:04:12
Imetengenezwa ndani: 
2012

Imetayarishwa na: 

FCI TV

Muhogo ni chakula kikuu barani Afrika na ubora wa vipandikizi vyake huathiri mavuno, na pia husababisha maambukizi ya wadudu na magonjwa. Kwa hivyo unahitaji kuwa muangalifu wakati wa kuchagua vipandikizi vya mihogo.

Vipandikizi vya mihogo vinapaswa kuchaguliwa kwa uangalifu. Vinapaswa kuwa na afya, vimekomaa vizuri, na urefu wa 30cm. Vipandikizi vinapaswa kuwa vinene ili kuhifadhi virutubisho vya kutosha na viwe na angalau vifundo 5. Mizizi na mashina kawaida hukua kutoka kwenye vifundo. Mimea ambayo vipandikizi hukatwa inapaswa kuwa kati ya miezi 6 hadi 18. Iwapo mmea una miezi 6, huwa laini, na machipukizi (vijicho) mengi ya kijani kibichi kumbe tunahitaji mashina magumu. Mashina lazima yasiwe na wadudu wala magonjwa ili mmea uweze kustawi vyema. Kwa hivyo kuna haja la kutibu mashina kabla ya kupanda.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:25Nyenzo za kupanda mihogo lazima zichaguliwe ipaswavyo. Lazima viwe vimekomaa, pamoja na afya, na urefu wa 30cm.
01:2601:39Vipandikizi vinapaswa kuwa vinene ili kuhifadhi virutubisho vya kutosha
01:4002:10Lazima viwe na angalau vifundo 5. Mizizi na shina kawaida hukua kutoka kwa vifundo.
02:1103:06Mimea unapaswa kuwa kati ya miezi 6 hadi 18
03:0703:38Vipandikizi lazima visiwe na magonjwa wala wadudu. Kwa hivyo kuhitaji matibabu kabla ya kupanda.
03:3904:12Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *