Nondo wa kantangaze ni wadudu waharibifu wa nyanya na husababisha hasara kubwa. Majaribio ya kuwadhibiti kwa njia ya kemikali sio tu kwamba hayajafanikiwa lakini pia huongeza gharama ya uzalishaji.
Kutumia dawa ya trianum, na mitego ya delta na tutasan ni hatua za kibayolojia za ulinzi wa mazao zinazotumiwa kudhibiti nondo wa kantangaze. Udhibiti wa kibayolojia ndio bora zaidi kwa wadudu hawa kwa sababu husaidia kutoa chakula chenye afya na usalama, hauachi kemikali kwenye mazao, hauathiri mazingira, gharama yake nafuu, na hulinda zao katika msimu mzima wa kilimo.
Mbinu za udhibiti
Trianum; hii huwekwa kama dawa ya kuzuia kuvu, ambayo hutumika kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na udongo kama vile fusarium na pyhthium. Dawa hizi huwekwa udongoni moja kwa moja wakati wa kupanda. Dawa hii huwekwa udongoni kwa kiwango cha kilo 1 kwa ekari.
Mtego wa maji wa tutasan hutumia dawa ya kuvutia wadudu inayoitwa pherodis pheromone. Pheromone huwavutia wadudu wa kiume ndani ya maji kwenye mtego ambamo sabuni iliongezwa. Sabuni huongezwa ili wadudu waweze kuzama ndani ya maji na kufa kwa urahisi. Mitego huwekwa kwenye chumba cha wavu (greehouse) baada ya kupandikiza kwa umbali wa mita 15 hadi 20 kati ya mitego. Kwa uwanja wazi, unahitaji hadi mitego 15 kwa ekari na inapaswa kusambazwa sawasawa. Badilisha dawa ya pheromone kila baada ya wiki 4 hadi 6.
Mtego wa Delta
The delta trap also works along with a pheromone but is basically for scouting and monitoring the Tuta absoluta to help the farmer know when to do the mass trapping of the pests. To use it, place the pheromone in the middle of the sticky plate and insert the plate on the delta then hang the setup in the field.