»Kutengeneza mboji ya minyoo«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=86S2WkZ7SCg

Muda: 

00:03:49
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

AgVid

Mboji ya mbolea huleta kipato kwa wakulima. Minyoo wa Kiafrika hukua hadi urefu wa inchi 5–6, wana uwezo wa juu wa kuzaliana, na pia huishi hadi miaka 2.5.

Hata hivyo, wakati wa mchakato huu, ongeza mboji ya minyoo iwapo minyoo hawapatikani ili kuwezesha mayai kuanguliwa. Ni muhimu kuweka saruji kwenye sakafu ili kudhibiti ndege, utitiri na panya kuingilia masanduku ya kutengenezea mboji ya minyoo, kwani wanaweza kuua minyoo. Zaidi ya hayo, jenga mfereji wa maji kuzunguka tanki, nyunyiza majivu ili kuzuia mchwa, usitumie viuatilifu na epuka mimea yenye harufu.

Hatua za kufuata

Chagua minyoo aina ya kiafrika kwa vile uwezo wao wa kuzaliana ni wa juu zaidi kuliko minyoo wa kisasa. Wotolee joto la kutosha kati ya nyuzi joto 25 – 30 Celsius, na unyevu wa asilimia 40 – 45%. Weka paa kwenye matangi ili kuzuia mvua na jua kuingia moja kwa moja kwenye mboji. Tangi linapaswa kujengwa kwa upana wa futi 3–4, kina cha futi 2–3 na urefu unaofaa.

Toboa tundu chini ya tangi ili kuondoa maji ya ziada na kukusanya mbolea ya minyoo ya maji. Weka safu ya nyenzo nzito chini mwa tangi, kisha ongeza safu ya nyenzo za kikaboni, pamoja na samadi ya mifugo na endelea kufanya utaratibu huo hadi tanki litakapojaa.

Weka hadi minyoo 25 juu ya nyenzo kwa kila futi ya mraba. Iwapo minyoo hawapatikani eneza mboji ya minyoo kwenye tanki kwa kuwa ina mayai ambayo yanaweza kuanguliwa.

Daima, nyunyiza maji juu ili kudumisha unyevu ndani ya matangi na hivyo kuhimiza maisha ya minyoo. Kusanya mboji ya juu, ikaushe ili kuondoa unyevu wa ziada, ichuje na kisha rudisha nyenzo kwenye tanki.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:14Kutengeneza mboji ya minyoo
00:1500:38Tumia minyoo ya Kiafrika na utoe halijoto, na unyevu wa kutosha.
00:3901:13Lisha minyoo kwa mabaki ya mazao, lakini epuka tumbaku na mabaki ya shambani mabichi.
01:1401:44Weka paa kwenye matangi. Tangi linapaswa kujenga kwa upana wa futi 3–4, kina cha futi 2–3 na urefu unaofaa
01:4502:03Toboa tundu chini ya tangi. Weka safu ya nyenzo nzito chini mwa tangi
02:0402:13ongeza safu ya nyenzo za kikaboni, pamoja na samadi ya mifugo na endelea kufanya utaratibu huo hadi tanki litakapojaa.
02:1402:31Weka hadi minyoo 25 juu ya nyenzo kwa kila futi ya mraba.Tandaza mboji ya minyoo juu.
02:3202:41Nyunyiza maji juu. Mbolea huwa tayari baada ya miezi 2–3
02:4203:05Kusanya mboji ya juu, ikaushe, ichuje na kisha rudisha nyenzo kwenye tanki.
03:0603:27Weka saruji kwenye sakafu na unyunyize majivu
03:2803:49Uzalishaji wa mboji ya minyoo huleta mapato.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *