Dairy farming is the keeping of cattle, goats and camels for milk production. The Friesian cow which is black and white and produces more milk than other breeds. ‚
Jersey, it is adaptable to extreme heat and cold conditions. Ayrshire has white and brown patches. Guernsey is fawn or red and white in colour. It is hardy and docile.
Kushughulikia idadi kubwa ya mifugo
Chunguza ng‘ombe kujua ni kiasi gani cha malisho anachoweza kula. Kulisha kunapaswa kufanywa kulingana na uzito wa mwili wa mnyama. Ng‘ombe wa Friesian atakula 3% ya uzito wa mwili wake. Mifano ya malisho ni pamoja na, nyasi ya napier, boma Rhodes, lucern, desmodium na majani ya viazi vitamu.
Kuchunguza ng‘ombe
Ng‘ombe wanapaswa kuwa wamepumzika, wanatafuna au wanakula. Ng‘ombe anaobaki nyuma wakati malisho yameletwa, wala hatafuni chochote, anaweza kuwa na tatizo. Ng‘ombe anapokuwa mlema, mtenganishe na ng‘ombe wengine, na umpeleke kwenye banda atibiwa mara moja.
Udhibiti wa wadudu
Punguza utembeaji wa wanyama, magari, na binadamu ndani na nje ya shamba. Wanyama wote wapya wanaojiunga na kundi wanapaswa kutengwa kwanza ili kuzuia kueneza magonjwa.
Tenganisha ng‘ombe walioathiriwa na kimeta, ugonjwa wa miguu na mdomo, na umjulishe daktari wa mifugo. Chanja ng‘ombe kila baada ya miezi 4 dhidi ya ugonjwa wa mguu na mdomo, na kila mwaka kwa ugonjwa wa kimeta.
Kukamua
Ukamuaji wa maziwa kwa kutumia mashine hupunguza gharama ya kazi na hufanya kazi bora. Kukamua kunapaswa kufanywa ndani ya dakika saba. Baada ya dakika 7 ng‘ombe huanza kutoa homoni ya oxytocin.
Mbinu duni za kukamua zinaweza kusababisha ugonjwa wa kiwele, ambao husababishwa na bakteria zinazoletwa wakati wa kukamua.