»Mbolea ya pumba za nazi (coir pith)«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/coir-pith

Muda: 

00:14:14
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Green Adjuvants

Coir ni nyuzi za maganda ya nazi zilizokomaa. Wakati wa usindikaji, tunapata bidhaa ya taka inayoitwa coir pith, ambayo huozeshwa na kutumika kama mbolea.

Mbolea hii ni muhimu sana katika maeneo ya ukame ambapo hasa kuna udongo wa kichanga, ili kuboresha uhifadhi maji ya udongo. Kwa kiasili, coir pith hupatikana kwa kuloweka maganda ya nazi ndani ya maji kwa wiki kadhaa. Kisha, maganda ya nazi huondolewa ndani ya maji na kupondwa kwa kijiti cha mbao. Baadhi ya wakulima huendesha trekta juu ya maganda ya nazi yaliyolowekwa, huku wengine wakitumia mashine. Kisha nyuzi hizo hutumika kutengeneza kamba, mikeka nakadhalika, huku pumba za nazi zikibadilishwa kuwa mboji.

Mchakato wa kutengeneza mbolea

Taka za maganda ya nazi huchujwa na kuwekwa kwenye eneo lililo na kivuli au mti ili kuoza. Rundo la mbolea hutengenezwa katika safu; tandaza safu ya kwanza ya takriban kilo 20 za nyenzo, na ongeza kiozaji kilicho na vijidudu vingi.

Kiozaji kinaweza kutengenezwa kwa kuchanganya lita 100 za maji na kilo 5 za samadi ya ng‘ombe, ndizi 10 zilizopondwa, lita 3 za mkojo wa ng‘ombe, nusu kilo ya sukari guru, nusu kilo ya unga, na kiganja kimoja cha udongo. Changanya haya na uyakoroge mara mbili kwa siku, kisha uyafunika na gunia. Baada ya wiki moja, hii itakuwa tayari kutumika.

Nyunyiza lita 10 za kiozaji kwenye safu ya pumba za nazi, kisha ongeza takribani kilo 4 za nyenzo iliyo na nitrojeni, kwa mfano samadi ya kuku.

Ongeza safu ya pumba za nazi, na kisha rudia mchakato. Gramu 100 za mbegu za uyoga au 100g trichodema zinaweza kutumika kama viozaji. Nyunyiza maji kwenye rundo kila siku ili kutunza unyevu. Fungua mbolea kila baada ya siku 10 ili kuingiza hewa safi. Mbolea itakuwa tayari baada ya mwezi mmoja.

Kutumia mbolea

Weka 100kg ya mbolea hii mwishoni mwa utayarishaji wa shamba. Kwa vitalu, changanya sehemu 1 ya mbolea na sehemu 4 za udongo kabla ya kujaza viriba au trei za mbegu.

Kwa miti ya matunda hadi miaka 10, weka 10kg kwa mmea kila baada ya miezi 6, na kwa miti ya matunda zaidi ya miaka 10, weka 15kg kwa mmea kila baada ya miezi 6.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0002:35Taka ya nazi inaweza kuozeshwa kuwa mbolea nzuri ya kikaboni.
02:3603:24Mbolea hii ni muhimu sana katika maeneo ya ukame ambapo hasa kuna udongo wa kichanga
03:2504:25Pumba ya nazi (coir pith) hupatikana kwa kuponda maganda ya nazi au kutumia mashine na trekta.
04:2604:56Nyuzi za nazi hutumika kutengeneza kamba, mikeka nakadhalika, huku pumba za nazi zikibadilishwa kuwa mboji
04:5705:23Kusanya pumba ya nazi na uichuje vizuri mpaka ili kuondoa nyuzi zote.
05:2405:42Chagua eneo lenye kivuli au chini ya mti ili kuozesha pumba za nazi
05:4306:45Rundo la mbolea hutengenezwa katika safu huku ukiongeza kiozaji kilicho na vijidudu
06:4608:20Nyunyiza lita 10 za kiozaji baada ya kilatabaka.
08:2108:20Mbegu za uyoga na trichodema zinaweza kutumika kama kiozaji.
08:2108:54Nyunyiza maji kwenye rundo kila siku ili kutunza unyevu.
08:5509:40Fungua mbolea kila baada ya siku 10 ili kuingiza hewa safi.
09:4111:51Kutumia mbolea shambani.
11:5214:14Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *