Kwa kuwa ni zao muhimu lenye lishe, tikitimaji hulimwa sana kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo, mbinu za usimamizi wake hazitekelezwi kikamilifu na wakulima, jambo ambalo hupunguza ubora na wingi wake.
Tikitimaji ni mboga ya jamii ya cucurbitaceae, na kitaalamu inajulikana kama cucmis melo. Tikitimaji ni mmea wa majani ambao hutambaa, na una machipukizi machanga yenye miiba ambayo hukua kutoka kwenye vijicho au mhimili wa majani. Mmea una mfumo wa mizizi nyingi ambayo hukua haraka.
Usimamizi wa tikitimaji
Mabua hupanda na kuenea, na yana vifundo ambapo majani, miiba na maua hukua. Pia, majani hukua kutoka kwenye shina kuu ambapo vijicho vya pili hutokezea na hubadilika kuwa chipukizi ambapo maua ya matunda ya kike huundwa.
Umbo la jani ni petiolated, palmate, alternate na limefunikwa na nywele chini, na limegawanyika katika vipande 3 au 7. Kingo za majani zimepindishwa kama msumeno. Maua ni ya rangi ya manjano, na yanaweza kuwa wa ya kiume, jike au huntha kulingana na mwonekano, aina ya mmea, halijoto, mwanga pamoja na mbolea iliyowekwa.
Maua ya kiume huonekana kwenye shina kuu siku 10–15 baada ya kupanda, huku maua ya kike yakionekana siku 10 baada ya maua ya kiume kutokea. Tunda la tikitimaji lina nyama na umbo lake hutofautiana na linaweza kuwa duara au mviringo. Ganda lake linaweza kuwa laini au kukwaruza, na rangi ya kijani, njano, uchungwa, au nyeupe. Tunda linapoiva nyama huwa nyororo, yenye maji maji, na rangi nyeupe au ya uchungwa kulingana na aina. Mbegu ni nyeupe au njano, umbo la mviringo, tambarare na ndefu.
Mmea wa tikitimaji huhitaji joto la wastani la nyuzi joto 18–26 ili kustawi, na unyevu wa kutosha wa 60–70% katika hatua ya kuchanua maua na kukomaa. Kuhusiana na unyevu wa udongo, mmea wa tikitimaji unahitaji kiasi fulani ili kuhimiza ukuaji wa majani na ukomaavu wa matunda.
Hata hivyo, unyevu kupita kiasi husababisha matatizo ya kuota na mara tu mmea unapoanza kukua matunda yatakuwa na ladha isiyo tamu.
Hatimaye, tikitimaji huhitaji udongo wa tifutifu wenye rutuba, usio twamisha maji , ambao una pH ya 5.5–7.2.