Kama mbinu za kilimo na usimamizi, upogoaji na uchavushaji wa mbiringanya kwa mikono huongeza ubora na wingi wa mazao na vile vile hali za kiuchumi.
Kupogoa hufanywa ili kuboresha tija ya mazao, na hasa hufanywa kwa kuondoa matawi na vikonyo vya ziada ili kuhimiza mzunguko wa mwanga na hewa. Hii hupunguza ushindani wa mwanga wa jua na madini.
Kupogoa biringanya
Wakati wa kupogoa, acha mashina 4 pekee ili kuepuka kupunguza kwa ubora na wingi wa matunda, pamoja na afya ya mmea. Unapopogoa, acha kwenye mmea maua yaliyochavushwa, na uimarishe shina la mmea kwa vijiti au kamba. Ondoa majani yote yanayochipuka chini ya shina la mmea kwa ajili ya kupalilia na kurutubisha mmea kwa urahisi.
Kamba za kuhimili au kuimarisha mimea zinapaswa kuwa legevu ili kuzuia kukata mmea wakati wa upepo mkali au mvua.
Uchavushaji wa mazao
Chavusha kwa mikono kwa kusugua sehemu ya ua ya kiume inayotoa chavuo (stamen) ili chavuo idondoke kwa sehemu ya ua yakike (pistil). Wakati mzuri wa kuchavusha ni asubuhi.
Hatimaye, tolea mmea mbolea ya madini na virutubisho.