Kipindi cha kutomkamua ng‘ombe wa maziwa hudumu kwa ujumla siku 60 kabla ya kuzaa.
Katika kipindi hiki, ng‘ombe huandaa kiwele chake kwa ajili ya kunyonyesha kwa hivyo shughuli hiyo ni muhimu sana kwa wafugaji. Usimamizi bora wa kipindi hiki husaidia katika udhibiti wa ugonjwa wa kiwele katika ng‘ombe.
Shughuli za kawaida
Daima fuata mbinu bora za kukamua , na vile vile epuka kukamua ng’ombe kighafla.
Zaidi ya hayo, wape wanyama virutubisho na madini ili kuboresha kinga yao dhidi ya magonjwa, pamoja na kupunguza matatizo baada ya kuzaa.
Kabla ya kuzaa, epuka kuwapa wanyama virutubisho vya kalsiamu na fosforasi.
Pia mlishe ng‘ombe aliye katika kipidi hicho chakula cha machangayiko, malisho ya kijani kibichi na wanga kwa ukuaji bora na afya bora.
Mwisho, usiwalishe wanyama kiwango cha ziada cha nishati mwishoni mwa kipindi cha kutowakamua.