Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa bata hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.
Ufugaji wa bata kibiashara una faida kubwa katika tasnia ya ndege, na unachukuwa nafasi karibu na ufugaji wa kuku ulimwenguni kote. Mtu yoyote anaweza kuuanzisha ufugaji wa bata kwa urahisi nyumbani. Bidhaa kama mayai na nyama zina wateja wengi katika soko la ndani na la kimataifa.
Usimamizi wa bata
Kwa vile ufugaji wa bata kibiashara ni chanzo kikubwa cha pesa, unaweza pia kuwa chanzo cha ajira. Kujenga banda la bata ni rahisi sana. Bata wanaweza kuhifadhiwa katika sehemu ya chini, ya iliyoinuliwa, nyevu, kavu, au sehemu nyingine yoyote. Unaweza pia kujenga banda kwa muundo rahisi, ambalo lazima liwe katika kivuli, na lizungushwe na uzio, na liwe na mifereji ya maji.
Kwa kawaida kila bata huhitaji nafasi ya futi 2–3 za mraba na katika hili, walinde dhidi ya wanyama wawindaji. Bata hula takiribani kila aina ya chakula na pia wana tabia asili ya kutafuta na kula chakula kama vile magugu, mwani, kunde, minyoo, konokono na wadudu.
Bata ni ndege ambao pia huishi kwenye maji, ingawa wanaweza kufugwa bila maji pa kuogelea. Hata hivyo, watolee maji ya kuchezea na kuloweka vichwa vyao. Bata wanaweza kuathiriwa na kiwango cha juu cha vifo kutokana na magonjwa yanayoenezwa kupitia bata aliyeambukizwa hadi mwenye afya. Magonjwa yanaweza kuzuilika na kudhibitiwa kwa kutumia mbuni za usalama na chanjo.
Kabla ya kuuza mayai, yasafishe na uyabebe kwa kutumia vikapu, trei na masanduku ya mbao.