Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa mbuzi hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.
Ufugaji wa mbuzi ni biashara yenye faida na huchangia lishe ya wafugaji na kuwatolea kipato. Mbuzi hutunzwa kwa urahisi. Usimamizi wa mbuzi hauhitaji vifaa vingi, mtaji mwingi au vibarua vingi.
Usimamizi wa mbuzi
Kwa usimamizi mzuri, tengeneza mpango mzuri wa biashara ya ufugaji mbuzi. Chagua eneo linalofaa ambalo lina vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji wa mbuzi ambavyo ni pamoja na maeneo yenye maji bora, vyanzo vya chakula, shamba lenye rutuba kwa ukuaji mzuri wa nyasi. Kulisha mbuzi malisho ya kijani hupunguza gharama za chakula na huwafanya wanyama kuwa na tija.
Vile vile, lazima kuwe na vibarua wa kudumu, usafirishaji bora na huduma za daktari wa mifugo. Pai jenga banda la mbuzi mahali palipo inuliwa ambapo maji ya mvua hayatatwama, na banda lazima liingize mwanga wa kutosha.
Sakafu ya banda lazima inuliwe futi 4–5 kutoka ardhini na paa liwe futi 6–8 kutoka kwa sakafu. Sakafu ya banda inapaswa kujengwa kwa mbao huku nafasi zikiachwa kati yazo ili kuruhusu mkojo na kinyesi kuanguka chini. Ili kulinda mbuzi dhidi ya kibaridi, weka damani za plastiki kwenye nyavu za madirisha.
Usimamizi mzuri wa malisho ya mbuzi ni muhimu kwa ufugaji wa kibiashara, kwani kwa kawaida mbuzi hula nyasi, vitamini na maji kwa ukuaji mzuri. Unahitaji ujuzi wa kutosha kuhusu ulishaji wa mbuzi, na usiwalishe chakula kilichochafuliwa au maji machafu, na pia safisha banda kila mara.
Tenganisha wanambuzi na tunza mbuzi wa kuzaliana na wajawazito. Ruhusu wanambuzi wawe na mama yao kwa wiki kadhaa baada ya kuzaliwa. Uhimilishaji bandia ni njia nzuri ya kuzaliana.
Chanja mbuzi kwa wakati, na dumisha uhusiano mzuri na daktari wa mifugo.