Biosecurite ni hatau zinazochukuliwa kudhibiti au kuzuia uenezaji wa magonjwa shambani, na inapaswa kuwa kipaumbele kwa wafugaji wa wa kuku.
Ili kufanikiwa na hatua hizo, lazima ziwe rahisi kutekelezwa na endelevu. Kudhibiti ugonjwa katika kundi la kuku kunaweza kufanywa kwa kutambua ugonjwa kwa urahisi, na kuchukua hatua za kuzuia uenezaji wa ugonjwa. Ili kuzuia uenezaji wa ugonjwa, lazima hatua za usalama zichukuliwe kwa mfano udhibiti wa uhamishaji wa mifugo, na kadhalika.
Hatua za kudhibiti au kuzuia uenezaji wa magonjwa
Hatua moja tu haiwezi kudhibiti uenezaji wa ugonjwa, hata hivyo kuna hatua jumuishi zinazoweza kufuatwa ili kuzuia na kudhibiti uenezaji wa magonjwa, ni pamoja na;
Kujenga uzio ili kuzuia watu kuingia shambani, kuwatolea kuku maji safi na chakula, na kuweka vizuizi vya ndege wa porini na panya kwenye banda la kuku.
Tumia mbinu jumuishi za usimamizi, badilisha nguo na viato wakati wa kuingia au kutoka kwenye banda la kuku.
Tenganisha ndege wapya, gawanya na kutenganisha mabanda, pamoja na kuyasafisha na kuua viini.
Mambo ya kimsingi ya kudhibiti au kuzuia uenezaji wa magonjwa
Hakikisha kwamba mabanda ya kuku na makazi ya watu yametenganishwa mbali na vyanzo vya magonjwa.
Dhibiti ufikiaji wa watu kwenye maeneo yaliyoathiriwa na magonjwa. Hii hunapunguza udhihirisho wa ndege kwa ugonjwa.
Dumisha usafi kwa kusafisha vifaa na makazi, pamoja na kudumisha usafi wa kibinafsi. Hatua hizi hazifai kuwa kamilifu 100% ili kudhibiti ugonjwa kwa ufanisi.