Watu wengi hufuga kuku kwa ajili ya mayai, na ikiwa kuku hawatataga au watataga mayai machache chini ya idadi inayotarajiwa, wafugaji hufadhaika.
Kuna sababu zinazozuia ndege kutaga mayai ipaswavyo. Sababu moja muhimu ni aina ya kuku. Aina ya kuku huathiri uzalishaji wa mayaia, kwa mfano; kuku ya mayai hutaga mayai mengi, na huanza kutaga katika wiki ya 22, na hutaga zaidi katika wiki ya 36 hadi wiki 56. Walakini, kuku wa kienyeji huchukua muda mrefu zaidi ya hapo kuanza kutaga, na hutaga idadi ndogo ya mayai.
Mambo ya usimamizi
Lishe: I wapo ndege wako hawali chakula sahihi, hawatataga au watataga mayai machache. Kuku wa mayai wanapaswa kulishwa chakula maalum kinacho chocheza uzalishaji wa mayai. Chakula hiki kinapaswa kuwa na kalsiamu nyingi.
Hali ya mazingira: Uzalishaji wa mayai ni mkubwa katika maeneo yenye joto ikilinganishwa na maeneo ya baridi. Wakati halijoto ya mazingira ni baridi banda la kuku pia huwa baridi, na hivyo uzalishaji wa mayai hupunguka kwa sababu chakula kikubwa kinacholiwa na ndege kitatumiwa kutolea mwili wa ndege joto.
Mpango wa kuasha taa: Tolea ndege wako mwanga wa kutosha ili kuongeza uzalishaji wa mayai, kwa sababu mwanga huwapa ndege masaa zaidi ya kula chakula. Hata hivyo mwangi mwingi kupita kiasi hupunguza ukubwa wa mayai.
Sababu za kiafya
Ndege wagonjwa hufadhaika, na hivyo chakula kingi hutumiwa katika uzalishaji wa chembechembe nyeupe za damu ili kupambana na ugonjwa. Baadhi ya madawa huwafanya ndege waache kutaga, kwa mfano ukitolea kuku dawa za kuua minyoo, hawatataga kwa siku tatu zijazo.
Hatua / umri wa ndege. Wakati ndege wanazeeka, uzalishaji wa mayai hupunguka.