Watu wengi hufuga kuku wa nyama lakini chakula ni kikwazo namba moja wanachokabiliana nacho. Hiki kinaweza kutatuliwa kwa kujitengenezea malisho yao wenyewe.
Ili kutengeneza mfuko wa kilo 70 wa chakula cha kuku wa mayai, unahitaji kilo 34 za mahindi, ngano, mihogo iliyosagwa na kilo 12 za soya iliyochomwa au kupikwa, samaki iliyosagwa kilo 8, wishwa wa mahindi kilo 10, wishwa wa ngano ili kuongeza ladha ya chakula, chokaa kilo 6, michanganyiko maalum kama vile lysine (70g), methionine (70g) na mwishowe nyenzo ambazo husaidia kupunguza athari za sumu inayopatikana kwenye malisho.
Chakula cha kuku wanaokua
Ili kutengeneza kilo 70 za chakula cha kuku wanaokua, unahitaji kilo 27 za mahindi/ngano, kilo 23 za wishwa wa mahindi/ ngano, kilo 3.4 za soya iliyochomwa au kupikwa, kilo 11 za alizeti au mbegu za pamba zilizosagwa. Viungo vingine ni pamoja na gramu 700 za unga wa mifupa, kilo 3 za chokaa na viambato vidogo ni pamoja na 50 g ya viondoa sumu, 14 g ya chumvi, 50g zinki na 50 g lysine.
Chakula cha vifaranga
Ili kutengeneza chakula cha vifaranga, unahitaji 31.5 mahindi/ngano, 9.1 kg ya wishwa wangano au mahindi, 7.72 kg ya unga wa ngano, 16.8 kg ya soya, 1.5 hadi 1.8g ya samaka waliosagwa, 1.5 kg ya chokaa na si zaidi ya 30 g chumvi.
Viungo vidogo kwa vifaranga ni pamoja na 60 g coccidiostat, 50g chick premix, 50 g ya vimeng‘enya, 50 g ya viondoa sumu na 10g ya methionine.
Tahadhari
Chakula kutoka kwa samaki waliosagwa kinapaswa kupikwa kabla ya kutumika, na mbegu za pamba lazima ziondolewe maganda.
Usizidi viwango vinavyopendekezwa vya mafuta hasa katika chakula cha kuku wa mayai kwa sababu hivyo hupunguza uzalishaji wa mayai.