Ufugaji wa kuku wa kienyeji au ufugaji wa kuku wa kienyeji walioboreshwa una faida kubwa. Hata hivyo, ni mradi mgumu kwani kwani unaweza kufaidika au kupata hasara.
Ni muhimu kutambua kwamba kuku huwa na asilimia fulani ya uzalishaji wa mayai katika umri fulani kulingana na aina yake.
Bidhaa za kuku za Kienyeji
Ni muhimu kuelewa kwamba mwishoni mwa mwaka utakuwa na bidhaa tatu za kuuza, yaani mayai, nyama na vifaranga. Kwa hivyo, ni muhimu kuzingatia soko la bidhaa.
Ili kufaulu katika ufugaji wa kuku wa kienyeji, elewa misimu ya bidhaa hizo tatu. Kwa mfano, mahitaji ya kuku ni ya juu sana kuanzia Aprili-Agosti. Kwa hivyo, unapaswa kuwa na kuku waliokomaa ambao watataga mayai wakati huo. Kwa wakati huu watu wanataka kununua mayai yenye rutuba kwa kuangua au kutotolesha vifaranga wa siku moja.
Kuongeza uzalishaji
Ili kupata mayai yenye rutuba yenye uwezo mkubwa wa kutotolewa, unapaswa kuwa jogoo mmoja kwa majike saba. Hii ina maana kwamba angalau asilimia 65–70% ya mayai yatarutubishwa. Hivi ndivyo unavyoweza kupata faida zaidi kwa kuuza vifaranga vya siku moja.
Unapouza mayai yenye rutuba, wafugaji wanaoangua mayai hayo watagundua kuwa mayai yako huanguliwa kwa asilimia kubwa na hivyo utapata soko kubwa la mayai.
Uwekezaji na utunzaji
Ufugaji wa kuku wa Kienyeji unahitaji mabanda ya kawaida, unanaweza kutumia mabati au mbao laini. Hii inakuwezesha kuwekeza zaidi katika idadi ya ndege au vifaa vya kutotolesha vifaranga.
Usikose kuchanja ndege wako. Ni muhimu kuzingatia mbinu bora za usimamizi kama vile kupunguza midomo, kuwapa dawa ya kuua minyoo, kubadilisha matandiko mara kwa mara na kuwapa ndege virutubisho vya vitamini baada ya kuwachanja. Pamoja na haya yote, weka rekodi ili kuchanganua na kujua wapi pa kuboresha.