Ugonjwa wa Covid-19 umeathiri mfumo wa chakula nchini Kenya. Ugonjwa huo umeathiri uazalishaji, ugavi na mahitaji ya chakula.
Usalama wa chakula ni sehemu muhimu ya utoshelevu wa chakula. Wizara ya kilimo inahimiza mbinu bora za kilimo na usalama wa chakula na mboga. Kemikali za kilimo ni bidhaa za zinazotumika kulinda mimea dhidi ya wadudu, na kuboresha ukuaji wao. Kemikali hizi ni pamoja na viuatilifu, viuawadudu, viuakuvu, viuavijasumu na mbolea za madini. Kemikali ni hatari kwa wanadamu, na kwa hivyo chukua tahadhari wakati wa kununua, kushughulikia na kuhifadhi dawa hizo.
Mavazi ya kujikinga
Unapotumia kemikali, vaa surupwenye, gumbuuti, miwani na barakoa. Kisha vaa kofia na hatimaye glavu.
Hakikisha kwamba surupwenye imevaliwa juu ya gumbuuti ili kuepuka kemikali kuingia kwenye miguu. Vaa glavu kwa mikono. Tayarisha kila kifaa kinachohitajika kabla ya kuchanganya dawa. Kuwa na udongo, brashi na ufagio. Pima kipimo cha dawa kilichopendekezwa.
Kuvuna mboga
Uvunaji wa mapema asubuhi ni bora kwa mazao mengi ya mboga, jua linapokuwa kali sana mmea hunyauka.
Tumia kisu kikali ili kuepuka kuharibu mmea. Acha angalau majani 4 kwa kila mmea, kwani mimea hutengeneza chakula kupitia majani. Vuna mara kwa mara, kwani huku kunaweza kusababisha ladha bora ya mboga na kuongeza mavuno.