Ugonjwa wa Covid-19 umeathiri mfumo wa chakula nchini Kenya. Ugonjwa huo umeathiri uzalishaji, ugavi na mahitaji ya chakula na michango.
Wizara ya kilimo mifugo na uvuvi imeanzisha bustani ya majiko milioni moja vijijini na mijini ili kukidhi majitaji ya chakula. Kuna njia kadhaa ambazo mtu anaweza kufuata ili kutengeneza bustani rahisi ya jikoni kwa kutumia nyenzo zinazopatikana nchini.
Bustani nyevu
Bustani nyevu ni mbinu ya uzalishaji wa mazao iliyoundwa ili kutoa hali bora ya unyevu wa udongo katika eneo dogo la uzalishaji. Kuna aina mbili za bustani nyevu; bustani iliyoinuliwa na bustani iliyozama ardhini.
Nyenzo zinazohitajika ni pamoja na; damani ya plastiki, waya, fito nne ndefu, udongo uliochanganywa na samadi kwa uwiano wa 1:1, mawa, nyasi kavu au taka za jikoni, mbao, mikasi, kifaa cha kumwagilia maji, na miche.
Kutengeneza bustani nyevu
Eneo lililochaguliwa lisiwe chini ya kivuli. Chukua vipimo vya bustani. Weka vijiti mahali ambapo fito zitawekwa. Chukua vipimo vya damani ya plastiki ambayo itatumika kutandika chini, hakikisha kwamba damani ya plastiki haina mashimo yoyote. Kata damani ya plastiki kwa mkasi, kata waya ambayo itatumika kufunga fito.
Tumia mawe kwenye msingi wa bustani ikiwa kuna maji mengi katika eneo hilo. Safu inayofuata ni nyasi kavu au taka ya jikoni kama kama vile mboga.
Kuongeza udongo
Ongeza udongo uliochanganywa na mbolea kwa uwiano wa 1: 1. Kina cha udongo kinapaswa kuwa 20–30 cm. Usiache nafasi ili kuepusha kupoteza maji wakati wa umwagiliaji.
Baada ya kutengeneza bustani, nyunyizia maji, panda mboga siku inayofuata.