Kuna njia kadhaa ambazo mtu anaweza kuanzisha bustani za jikoni kwenye nafasi ndogo kwa kutumia vifaa vya kienyeji.
Bustani hizi ni pamoja na bustani ya koni, bustani ya ghorofa nyingi, bustani ya magurudumu, bustani nyevu na bustani ya matone. Bustani ya matone ni mbinu rahisi ambayo huchukua muda kidogo na kibarua kidogo kutunzwa.
Bustani ya umwagiliaji wa matone
Nyenzo zinazotumika ni pamoja na: dumu za plastiki, chupa ya lita 5, ufito, sindano, misumari, udongo uliochanganywa na samadi kwa uwiano wa 1:1, maji na miche.
Bustani inapaswa kuwa katika eneo ambapo haizui chochote. Weka bustani kwenye ukuta au ufito kwa urefu ambapo unaweza kufikia kwa urahisi. Kwenye ufito, pima mahali ambapo utaninginiza dumu ya maji, kwa urefu wa 50cm. Panga dumu hizo kwa njia mbadala.
Kutengeneza mfumo rahisi wa umwagiliaji wa matone
Kata dumu, ondoa sehemu ya chini na toboa mashimo machache kwenye pande zote mbili. Weka msumari wa inchi 3–4 ili kushikilia dumu kwenye ufito, kisha weka dumu. Tumia waya ili kufunga vizuri dumu kwenye ufito. Hakikisha kwamba dumu limethibitishwa vizuri ili mazao yasianguke.
Kuweka udongo
Weka mawe ili kuzuia udongo kumwagika kutoka kwenye dumu. Jaza dumu kwa udongo. Pata chupa ya lita 5 na tumia sindano ili kutoboa mashimo madogo chini ya chupa ambayo yatamwagilia maji. Kisha jaza maji kwenye chupa na uifunge. Funga waya kwenye shingo la chupa na uning‘inize chupo hiyo kwenye msumari.
Jaza dumu na maji ili maji yadondoke na udongo upate unyevu wa kutosha. Dumu hilo linaweza kubeba hadi mimea mitatu.