Katika kampuni ya Eco Makaa solution, wanabadilisha takataka kuwa mkaa ya briketi. Mtu anaweza kubadilisha takataka kuwa mkaa ya briketi na kuokoa mazingira kutokana na uchafuzi.
Ili kuanza kuzalisha mkaa ya briketi, mambo yafuatayo yanazingatiwa. Kwanza ni nyenzo, na katika hii aina ya taka za majani ya kutumika izingatiwe. Pili, unapaswa kuangalia mashine zinazohitajika na upatikanaji wazo. Mwisho ni mtaji, kwaani ni muhimu sana kuwa na mtaji wa kuanzisha biashara. Mtaji unaweza kupatikana kutoka kwa akiba, marafiki au mikopo. Eco makaa solutions inatoa mafunzo bila malipo ili kuboresha maisha ya watu.
Mchakato wa uzalishaji wa makaa ya briketi
Hatua ya kwanza ni kuchoma taka ili zibadilike kutoka rangi ya kahawia hadi nyeusi.
Kisha, nyenzo zinazopatikana huchujwa ili kupata vumbi la mkaa. Maganda ya mpunga huongezwa kwenye vumbi la mkaa na kuchanganywa pamoja. Kisha molasi huongezwa ili kuunganisha nyenzo. Kisha nyenzo huunda katika umbo na urefu sahihi kwa kutumia mashine.
Shughuli zaidi
Briketi nyevu kisha hupangwa katika muundo wa pembetatu, na bidhaa ya mwisho huchukuliwa na kukausha. Makaa ya briketi huchukua siku 2–3 kukauka kwenye jua.
Briketi nyevu hutandazwa pamoja kwenye mstari ili kupata mwangaza wa juu wa kutosha kuzikausha. Kiunganishi kilichoongezwa husaidia briketi kutovunjike, na pia mashine ina uwezo wa kusaidia katika hili.
Mambo ya kimazingira ya ziadi
Makaa ya briketi hayana moshi, hutoa moto zaidi kuliko makaa ya kuni, vilevile na hayaharibu mazingira kwa vile hayatoi moshi. Pia mkaa ya briketi ni ya kiuchumi na huokoa pesa, kwaani yanaweza kuaka hadi masaa sita.
Mwanzilishi wa Eco makaa solution anashauri vijana wa Kenya, wanawake na watu wasio na ajira kujiunga na Eco makaa ili kujifunza kutengeneza mkaa ya briketi.