Mmomonyoko wa udongo ni miongoni mwa changamoto kubwa zaidi kuhusu usalama wa chakula duniani.
Usimamizi duni wa maeneo ya malisho na mbinu duni za kawaida za kilimo kama vile kupanda zao hilo hilo kila msimu, na kutorejesha upya taka za kikaboni huacha udongo wazi. Upepo na mvua basi husababisha mmomonyoko wa udongo kwenye mashamba ya miteremko.
Kupunguza mmomonyoko wa udongo
Mitaro na matuta ndizo njia zinazotumiwa sana kudhibiti mmomonyoko wa udongo. Mitaro hujengwa kwa kuchimba mishimo bwavuni mwa muinuko wa ardhi na kwa kuweka udongo kwenye upande wa chini wa kilima. Huku huwezesha mtiririko wa maji kukusanywa kwenye mitaro na maji haya yanaweza kupenya vyema ardhini.
Matuta yanafanana kabisa na mitaro. Pia hujengwa bwavuni mwa muinuko wa ardhi kwa kutengeneza upya mteremko kuwa madaraja mengi ambayo kwa kawaida huimarishwa kwa mawe. Mtiririko hupunguzwa kasi, na hivyo maji huwa na muda wa kutosha kupenyeza ardhini.
Mimea kama vile nyasi lazima ipandwe kwenye matuta tangu mwanzo.
Kujenga matuta ya kuishi
Ili kujenga mtaro hai, safu za miti hupandwa bwavuni mwa muinuko wa ardhi. Wakati miti imekua hadi urefu wa mita kadhaa, hukatwa na kuwekwa kimlalo kati ya vikonyo vya miti ili kupata muundo wima na wa usawa.
Kwa kuchagua miti ambayo huenezwa na vipandikizi, matawi yaliyokatwa yataunda mizizi wakati yanapogusana na udongo, na kwa njia hii muundo wote utakuwa hai, na imara zaidi kutokana na mizizi.