»Jinsi ya kuchapa alama kwenye nyuki malkia«
Watu wengi hutumia kalamu za kuchapa alama ambazo kwa kawaida husafishwa baada ya muda. Jambo hilo hutatiza sana wafugaji wa nyuki wakati wakimtafuta tena malkia ili waweze kumchapa alama upya.
Ni bora kupata rangi ya gari na brashi ndogo ambayo unaweza kutumia kuweka alama nyuma ya malkia. Rangi ya gari hufanya kazi vizuri zaidi kuliko kalamu wakati imekauka. Vinginevyo, unaweza kutumia kalamu za tona ambazo daima husababisha ubora mzuri endapo unaweka alama kwenye nyuki malkia. Kuna aina mbalimbali za rangi za kuchagua na kwa hiyo tumia rangi zinazoweza kuonekana katika misimu tofauti. Daima hakikisha kwamba rangi unayoichagua hustahimili hali mbalimbali za hewa. Ikiwa unataka kumweka alama malkia na kalamu ya rangi, daima tumia kalamu ya mafuta.
Mbinu
Kuna njia nyingi za kumkamata malkia ili kuweka alama, kwani watu hutumia zana na njia tofauti katika mchakato huu. Hata hivyo, matumizi ya ngome huhakikisha usalama na uwekaji rahisi wa alama. Hii ni mbinu ambayo imechukuliwa na kujifunzwa na watu wengi.
Kuweka alama kwenye malkia
Tambua malkia na umtenganishe na wengine. Kisha muweke ndani ya ngome ambayo ina mashimo yasiyomruhusu kutoroka.
Tumia ncha ya kalamu ili kuweka alama mgongoni mwa malkia kwa uangalifu ili asimuumize huku akiwa ndani ya ngome. Acha rangi ikauke kwa takriban dakika 5 kabla ya kumwachilia.
Vikwazo
Ukiondoa ngome mara moja, nyuki vibarua watarudi moja kwa moja ndani na kumsafisha malkia jambo ambalo litafanya kazi yako kutokuwa na ufanisi.
Daima hakikisha kwamba wakati wa mchakato huo, hauui malkia. Ni afadhali kuwa na malkia asiye na alama aliye hai kuliko aliye na alama aliyekufa . Kwa hivyo, jifunze kwa umakini njia za kumfungia malkia ndani ya ngome bila kumuathiri.