“Nyuki huhitaji nafasi yipi ndani ya mzinga- Jinsi ya kupanua nafasi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=wHTOmo5Ah4o

Muda: 

09:02:00
Imetengenezwa ndani: 
2023

Imetayarishwa na: 

Black Mountain Honey

“Nyuki huhitaji nafasi yipi ndani ya mzinga- Jinsi ya kupanua nafasi”

Kuongeza sanduku juu ya mzinga ili kupanua nafasi ni jambo muhimu, na lazima hilo lifanywe katika wakati sahihi. Unaweza kufanya huku kwa kutumia njia tofauti ingawa watu wengi huweka masanduku zaidi.
Kuweka  masanduku mengi zaidi kwenye mzinga mdogo huathari ufugaji wa nyuki, kwani nafasi ambapo nyuki watafanyia kazi itakuwa paana sana kuliko inavyofaa. Mara sanduku la kutotoleshea limejaa, ongeza sanduku lingine juu ya mzinga. Ukifungua kisanduku na takriban fremu 100 zimejaa na masega, kuna uwezekano mkubwa kwamba fremu mbili za nje zitakuwa zimejaa asali. Hivyo ndivyo tu nyuki wanavyojenga viota vyao ili wawe na asali kwenye kingo za nje za viota. Unapogundua kuwa nyuki wako hawaingii kwenye kisanduku cha juu, jua kwamba hakuna nyuki wa kutosha ndani ya mzinga.

Utaratibu

Njia bora ya kuwafanya nyuki waende kwenye kisanduku cha juu ni kutumia sega maalum yaliyojengwa ndani ya mzinga.
Nyuki hupendelea sana masega haya. Kwa hivyo, ikiwa hauna masega haya, pata kipande kimoja au viwili vya sega lolote na uliweke katikati mwa sanduku na hilo litasaidia kuvutia nyuki kuingia ndani mwa sanduku la juu.

Mahitaji

Ongeza kisanduku juu ya mzinga mapema sana iwezekanavyo. Pata kipande cha sega na ukiweke katikati ya kisanduku. Hakikisha kwamba unaacha nafasi ifaayo kati ya fremu  za mzinga.
Unapogundua nyuki kwamba nyuki wameingia kwenye kisanduku cha juu, ongeza kingine huku ukihakikisha kwamba  kuna nafasi ya kutosha kufanya shughuli nyingine za mzinga. Usiruhusu nyuki kufikia juu ya mzinga.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:15Kuongeza sanduku juu ya mzinga ili kupanua nafasi ni jambo muhimu
01:1602:20Mara sanduku la kutotoleshea limejaa, ongeza sanduku lingine juu ya mzinga.
02:2103:10Unapogundua kuwa nyuki wako hawaingii kwenye kisanduku cha juu, jua kwamba hakuna nyuki wa kutosha ndani ya mzinga.
03:1104:20Njia bora ya kuwafanya nyuki waende kwenye kisanduku cha juu ni kutumia sega maalum yaliyojengwa ndani ya mzinga.
04:2105:30Sababu ya kuongeza kisanduku cha juu
05:3106:20Ukubwa wa mzinga
06:2107:20Acha nafasi ya kutosha kati ya fremu
07:2108:05Unapogundua nyuki kwamba nyuki wameingia kwenye kisanduku cha juu, ongeza kingine
08:0609:02Epusha vifo vya nyuki kwa kuongeza nafasi

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi