Kwa nini nyuki hutoroka? Kubomoa mzinga wa nyuki asili wa Kijapani

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=HgnqYoSEcag&t=110s

Muda: 

09:14:00
Imetengenezwa ndani: 
2022

Imetayarishwa na: 

Japanese natural beekeeping
Kundi la nyuki ambalo lilikuwa limeanzishwa linaweza kutoroka mzinga. Kundi hilo linaweza kubomolewa baada ya nyuki kulitoroka.
Sega hunganishwa kwenye ubao mwembamba ambao umeunganishwa pia kwenye dari chini ya kivuli, kwa hiyo tutaanza kwa kuondoa ubao. Kwanza, tunalegeza nta iliyounganishwa kwenye ubao na dari. Tunaweza kuondoa sega bila kuva vaazi lolote la kinga wakati wa joto, lakini ni vaa vazi hilo nyuki wanapofadhaika. Tunatengeneza pengo kati ya dari na ubao ili kulegeza sega. Baadhi ya masega yalikuwa na asali hapo awali, lakini nyuki walichukua asali walipotoroka. Kuna mabuu.
Ufafanuzi
Hapo awali, kundi hili lilikuwa katika mzinga wa kienyeji wa Kijapani lakini lilihama. Eneo jepesi la sega ni jipya zaidi huku eneo jeusi ni zee. Sehemu nyepesi ya sega ilijengwa baada ya kundi kuhamishwa. Kuna nyuki wengi kuliko tulivyotarajia kwa hivyo inawezekana kwamba nyuki waliobaki walikuwa wametoka kuchukua nekta asubuhi hiyo na wakati wanarudi kundi lilikuwa tayari limetoroshwa. Kutoroka kulitokea haraka sana na kulidumu kama dakika tano tu. 

 Kuondoa sega

Tutalipuliza moshi kwa upole ili baadhi ya nyuki waondoke kabla ya kulibomoa kundi. Kisha tuweke sega lenye asali kwenye chombo cha plastiki. Ondoa sega kwa uangalifu, epuka kuumiza au kuua nyuki. Anafanikiwa kutoa sega zima na anaweza kuona asali iliyohifadhiwa kwenye sega. Katika sega la tatu ambalo lilitolewa, tulipata mayai kwenye mabuu. Hii inaonyesha kwamba nyuki hawakupanga kutoroka mapema. 

Sababu za nyuki kutoroka mzinga

Malkia alikuwa bado akitaga mayai hadi kutoroka. Malkia anaonekana kuwa na afya njema na hakuna dalili ya ugonjwa. Sababu inayowezekana zaidi ya nyuki kutoroka ilikuwa usumbufu wa kurekodi filamu mara kwa mara. Wakati mwingine dubu hushambulia nyuki za Kijapani. Kutoa sauti maalum ni njia ya ulinzi ambayo nyukihutumia kuwatisha wanyama, kama vile dubu. Kikundi mara nyingi kingeonyesha mbinu hii wa ulinzi wakati wowote upigaji picha ulipokuwa unafanyika. Inawezekana kwamba nyuki walituona sisi kama dubu na wakaamua kutoroka kwani huenda nyuki waliamini kwamba wangeweza kushambuliwa.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:44Kundi la nyuki ambalo lilikuwa limeanzishwa linaweza kutoroka mzinga. Kundi hilo linaweza kubomolewa baada ya nyuki kulitoroka.
00:4502:15Sega hunganishwa kwenye ubao mwembamba ambao umeunganishwa pia kwenye dari chini ya kivuli, kwa hiyo tutaanza kwa kuondoa ubao.
02:1603:46nyuki huchukua asali walipotoroka.
03:4705:17Baada ya kutenganisha sega kutoka kwa ukuta, bomoa sega
05:1806:32Asali iliyotengenezwa katika majira ya masika ina ladha kali.
06:3307:44Uwepo wa mayai na mabuu unaonyesha kwamba nyuki hawakupanga kutoroka mapema
07:4509:14 Sababu inayowezekana zaidi ya nyuki kutoroka ilikuwa usumbufu wa kurekodi filamu mara kwa mara

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi