Kukaushia kwa jua ni nbinu ya kienyeji ya kukausha mpunga ambayo huhitaji uwekezaji mdogo na haiathiri mazingira.
Vipima joto na vipima unyevu vinaweza kutumika kupima joto na unyevu wa nafaka mtawalia. Kukaushia nafaka kwa jua kuna faida kadhaa kwamba; ni nafuu, hakuathiri mazingira, wala hakusababishi uchafuzi wa mazingira.
Mchakato wa kukaushia mpunga kwenye jua
Tandaza nafaka juu ya sehemu ya kukaushia katika mahali penye hewa nzuri huku ukichanganya nafaka kila baada ya dakika 30 ili ziweze kukauka haraka. Angalia halijoto ya nafaka na unyevunyevu kwa kufunika mpunga ikiwa halijoto ni zaidi ya nyuzi joto 50.
Kusanya nafaka ikiwa mvua itanyesha na pia usiku ili kuzuia nafaka kunyonya unyevu na kupasuka. Punguza unyevu hadi 18% kwenye safu ya nafaka ya nje ili kurahisisha uhifadhi kwa wiki 2 kabla ya kutumia mfumo mwingine wa kukausha. Mwishowe, kila wakati zuia wanyama kufikia nafaka, na epuka kukaushia kwenye barabara kwani huku kunaweza kusababisha uchafuzi wa nafaka.
Mapungufu ya kukaushia juani
Kukaushia juani huchelewesha mchakato wa mbegu kukauka. Na pia haiwezekani kukausha nafaka wakati wa mvua au usiku, jambo ambalo husababisha ukuaji wa ukungu. Pia ni ngumu kudhibiti halijoto kwajoto kali hupunguza ubora wa nafaka.
Mbinu za kukaushia juani
Kukaushia shambani; huku kunafanywa kwa kuweka mimea iliyokatwa juu ya ardhi au kwenye kininginizio, kwa vile nafaka zinaweza kupata unyevu usiku, ubora wazo huwa duni.
Kukausha gunzi; huku kunafanywa kwa kuweka gunzi zilizofungwa pamoja kwenye mikeka, sakaf au jukwaa, hata hivyo gunzi hukauka polepole.
Kutumia wavu au mikeka kukausha; huku hutekelezwa na wakulima wadogo kwa kuweka nafaka kwenye wavu na mikeka. Hata hivyo, gharama za kununua wavu na mikeka ni ghali, pamoja na changamoto la uchafuzi kutoka ardhini.
Kukaushia sakafuni; huku hutekelezwa na wakulima wakubwa kwa kutandaza nafaka kwenye sakafu, hata hivyo ni kazi ngumu zaidi ambayo pia huhusisha uchafuzi.