Nondo wa hariri hula tu majani ya mmea fulani unaoitwa mnyoyo. Ili kufuga nondo wa hariri kwa kiwango kikubwa, unahitaji kupanda miti ya mnyoyo ya aina tofauti kwa kiwango kikubwa.
Aina maarufu za mnyoyo
Aina maarufu za mnyoyo ni pamoja na mnyoyo wa Pakistan ambayo una matunda makubwa sana hadi inchi 2.5 kwa urefu, matunda yake ni matamu sana.
Mnyoyo aina ya collier ambao ni mseto wa mnyoyo mweupe na mwekundu. Una matunda ya zambarau yenye ladha tamu.
Mnyoyo aina ya Kirusi ambao una tunda jekundu – jeusi kwenye. Mti wake ni mrefu na hustahimili ukame, na mara nyingi hupandwa kwa ajili ya wanyamapori au vizuia upepo.
Illinois everbearing aina ambayo ni mseto wa mulberry nyeupe na nyekundu. Matunda meusi, matamu na makubwa kutoka kwa mti wenye matunda mengi.
Mnyoyo aina ya rivera ambao ni zambarau-nyeusi, tamu sana na matunda yaku huchukua muda mrefu kuiva.
Kilimo cha mnyoyo
Pata vipandikizi vyema vya mnyoyo na uvipande kwa umbali wa futi 3 kwa 3.
Rutubisha udongo kwa mboji na matandazo ili kuweka udongo unyevu sawa.
Kata miti michanga ili kuwezesha mmea kutoa matawi yenye nguvu..
Palilia ili kuzuia magugu shambani na baada ya miezi 6, mkulima anaweza kuvuna. Kwa wakati huu, mavuno hayatoshi na yanaendelea kuongezeka hadi miaka 2 hadi 3.
Ufugaji wa nondo wa hariri
Ili kuanza ufugaji wa nondo wa hariri, unahitaji kwanza kupanda mnyoyo kwa ajili ya malisho ya nond. Jenga chumba cha kawaida cha ufugaji ambacho ni 30 ft kwa 20 ft na hiki kinaweza kutunza nondo 40,000.
Baada ya hayo, pata mafunzo juu ya kufuga nondo wa hariri.
Anza kufuga nondo wa hariri kutoka kwa mayai au mabuu ya nondo.
Nondo wa hariri hubadilika kabisa ingawa mabuu hutimiza hatua 5 tofauti za ukuaji.
Nondo dume na jike waliokomaa huwekwa mahali palipotengwa ili wajamiane kwa saa 10, na baadaye hutenganishwa. Jike hutaga mayai huku la kiume likifa.
Baada ya kutaga mayai, mayai hutiwa asidi na formalin ili kulainisha ganda la yai ili kuwezesha kuanguliwa.
Usindikaji wa hariri
Baada ya kuvuna vifuko, vifuko huchemshwa ili kuyeyusha gamu.
Kishas viuko kubadilishwa kuwa nyuzi, lakini hilo hutegemea aina ya kitambaa unachohitaji kutengeneza.