Kilimo msetu cha mpupu kina manufaa nyingi. Kilimo hiki huboresha udongo kwa kutoa virutubisho na nitrojeni. Kunde la mpupu hufunika ardhi na kwa hivyo huilinda dhidi ya mmomonyoko, pamoja na kuboresha mavuno hata katika miaka ijao.
Wakulima wengi hukuza mihogo pamoja na mahindi mwanzoni mwa msimu mkuu wa mvua. baadhi ya wakulima hukuza mahindi katika msimu wa pili wa mvua, Lakini kwa sababu mvua haitabiriki, wakulima huvuna mavuno machache, au hata kukosa kabisa. Kwa sababu ya kuendelea kulima bila kufanya chochote kuboresha udongo, ardhi huchoka na mavuno katika msimu mkuu hupungua.
Kuhusu mpupu
Sawa na mbaazi na maharagwe, mpupu ni jamii kunde inayoweka nitrojeni kwenye ardhi kutoka hewani . Kwa kawaida, nitroheni hii huhafidhiwa katika majani na mbegu. Lakini mimea inapovunwa, nitrojeni nyingi huondolewa shambani.
Mbegu ya mpupu (upupu) haiwezi kuliwa na wanadamu jinsi ilivyo. Mashina yake yanaotambaa huzaa majani mengi, na mbegu zake hubaki shambani ili kurutubisha ardhi. Mpupu husaidia kuondoa aina nyingi ya magugu kama vile kiduha na nyansi aina ya mtimbi (imperata).
Jinsi ya kupanda mahindi na mpupu.
Mpupu hupandwa katikati ya mistari ya mahindi wakati wa msimu mkuu wa mvua. Ili ishike vizuri, anza kwa kupanda mahindi katika mistari. Acha upana wa sentimita 80 kati ya mistari, na sentimita 40 kati ya mahindi. Kutumia kamba zilizo alama ya umbali hurahisisha kazi. Dondosha mbegu mbili za mahindi katika kila shimo la kupandia. Ili kuzuia mpupu usifungefunge mahindi yako, panda mpupu wakati mahindi yamefikisha siku 60. Ni muhimu kumwagilia maji shambani kabla ya kupanda mpupu.
Panda takribani kilo 60 za mbegu za mpupu katika hekta mokaja ya mahindi, ili kuhakikisha kuwa udongo utafunikwa vizuri. Dondosha mbegu mbili kwa kila tuta kwa sentimita 40 kati ya mistari ya mahindi.
Baada ya kuvuna mahindi, mpupu huendelea kukua hadi mwisho wa msimu mfupi wa mvua. Mtandazo mzito wa mpupu huoza na kusaidia kuhifadhi unyevu wa udongo wakati wa kiangazi. Kutegemea wingi wa magugu, panda mahindi kwenye mpupu bila kulima shamba.