Uyoga chaza ni kuvu inayoliwa na inakidhi mahitaji ya kila siku. Kukuza uyoga chaza kunahitaji shamba kidogo, juhudi kidogo na pesa kidogo. uyoga chaza unaweza kutumika kupata pesa nyumbani.
Kuandaa mahali pa kukuza uyoga (msingi)
Uyoga chaza unaweza kukua kwa magogo na majani yaliokauka, lakini pia kwenye vifaa vya upanzi kutoka kwa mimea yenye nyuzi. Kwa hivyo unaweza kutumia mabua ya nafaka, mabaki ya mahindi, mabaki ya maharagwe, mabaki ya nazi, gugu maji, majani ya ndizi yaliokauka, na nyuzi za mnazi.
Maandalizi ya msingi hufanywa kwa njia hii: Tandaza msingi kwenye demani ya plastiki na ongeza maji yaliyochanganywa na kumvi ya mtama au molasi ili kuongeza virutubisho. Pia ongeza maji ya chokaa ili kupunguza asidi kwa msingi. Finya kiasi kidogo cha msingi kwa mkono ili kukagua iwapo msingi una unyevu wa kutosha.
Weka msingi kwenye mifuko ya plastiki, iliyo na rangi yoyote na ukubwa wowote. Bora isiwe na mashimo yoyote. Jaza mifuko kabisa ili kuzuia kuwa na nafasi. Kisa, funga mifuko.
Pasha moto msingi kwa angalao masaa 2 ili kuua viini. Baadaye, acha msingi kupoa ikiwa katika mahali safi.
Kupanda uyoga
Weka mbegu kwenye msingi uliyo katika mifuko ya plastiki, na uifunge ukiacha nafasi kidogo ili kuruhusu hewa kuingia. Weka pamba iliyopakwa na spiriti ili kuzuia viini. Katika kila mfuko, weka kijiko cha mbegu za uyoga juu ya msingi. Unaweza kununua mbegu za uyoga kutoka kwa taasisi ya utafiti, chuo kikuu au kutoka kwa mkulima wa uyoga. Weka mifuko kwenye chumba chenye giza, kilicho baridi ili mbegu ziweze kuenea.
Angalia na ufungue mifuko ili kuona iwapo msingi umefunikwa kabisa kwa uweupe wa mbegu. Nyunyizia maji anagalao mara 3 kila siku ili kupunguza joto na kuongeza unyevu.
Vuna uyoga wote kutoka kwa msingi ili kudhibiti nzi, panya na konokono. Hakikisha kwamba uyoga uko safi, laa sivyo, utaharibika.