»Kukuza uyoga chaza«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/growing-oyster-mushrooms

Muda: 

00:11:55
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

KENAFF

Uyoga chaza ni kuvu inayoliwa na inakidhi mahitaji ya kila siku. Kukuza uyoga chaza kunahitaji shamba kidogo, juhudi kidogo na pesa kidogo. uyoga chaza unaweza kutumika kupata pesa nyumbani.

Kuandaa mahali pa kukuza uyoga (msingi)

Uyoga chaza unaweza kukua kwa magogo na majani yaliokauka, lakini pia kwenye vifaa vya upanzi kutoka kwa mimea yenye nyuzi. Kwa hivyo unaweza kutumia mabua ya nafaka, mabaki ya mahindi, mabaki ya maharagwe, mabaki ya nazi, gugu maji, majani ya ndizi yaliokauka, na nyuzi za mnazi.

Maandalizi ya msingi hufanywa kwa njia hii: Tandaza msingi kwenye demani ya plastiki na ongeza maji yaliyochanganywa na kumvi ya mtama au molasi ili kuongeza virutubisho. Pia ongeza maji ya chokaa ili kupunguza asidi kwa msingi. Finya kiasi kidogo cha msingi kwa mkono ili kukagua iwapo msingi una unyevu wa kutosha.

Weka msingi kwenye mifuko ya plastiki, iliyo na rangi yoyote na ukubwa wowote. Bora isiwe na mashimo yoyote. Jaza mifuko kabisa ili kuzuia kuwa na nafasi. Kisa, funga mifuko.

Pasha moto msingi kwa angalao masaa 2 ili kuua viini. Baadaye, acha msingi kupoa ikiwa katika mahali safi.

Kupanda uyoga

Weka mbegu kwenye msingi uliyo katika mifuko ya plastiki, na uifunge ukiacha nafasi kidogo ili kuruhusu hewa kuingia. Weka pamba iliyopakwa na spiriti ili kuzuia viini. Katika kila mfuko, weka kijiko cha mbegu za uyoga juu ya msingi. Unaweza kununua mbegu za uyoga kutoka kwa taasisi ya utafiti, chuo kikuu au kutoka kwa mkulima wa uyoga. Weka mifuko kwenye chumba chenye giza, kilicho baridi ili mbegu ziweze kuenea.

Angalia na ufungue mifuko ili kuona iwapo msingi umefunikwa kabisa kwa uweupe wa mbegu. Nyunyizia maji anagalao mara 3 kila siku ili kupunguza joto na kuongeza unyevu.

Vuna uyoga wote kutoka kwa msingi ili kudhibiti nzi, panya na konokono. Hakikisha kwamba uyoga uko safi, laa sivyo, utaharibika.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:56Uyoga chaza ni kuvu inayoliwa na inakidhi mahitaji ya kila siku
00:5701:12Uyoga chaza hula magogo na majani yaliyokauka
01:1301:31Uyoga una protini, vitamini, nyuzi na madini, na unaweza kupandwa nyumbani.
01:3202:12Kukuza uyoga chaza kunahitaji shamba kidogo, juhudi kidogo na pesa kidogo.
02:1302:59Kuandaa msingi wa kukuza uyoga, kupanda na kuzalisha uyoga.
03:0003:14Tandaza msingi kwenye demani ya plastiki
03:1503:50Ongeza maji yaliyochanganywa na kumvi ya mtama au molasi na chokaa.
03:5104:05Kukagua iwapo msingi una unyevu wa kutosha.
04:0605:14Pasha msingi moto kwa angalao masaa 2 ili kuua viini.
05:1505:25Acha msingi kupoa ikiwa katika mahali safi.
05:2606:14Hakikisha mikono na nguo zako ni safi, na tumia kemikali kidogo
06:1507:03Weka mbegu kwenye msingi.
07:0407:22Funga mifuko ukiacha nafasi kidogo ili kuruhusu hewa kuingia. Weka pamba iliyopakwa na spiriti.
07:2307:52Weka mifuko kwenye chumba chenye giza.
07:5308:14Angalia na ufungue mifuko ili kuona iwapo msingi umefunikwa kabisa kwa uweupe wa mbegu.
08:1508:54Nyunyizia maji anagalao mara 3 kila siku ukitumia bomba la mkono.
08:5509:05Vuna uyoga wote kutoka kwa msingi.
09:0609:24Dhibiti nzi, panya, na konokono.
09:2510:08Baadaye, tumia msingi kama mbolea.
10:0911:55Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *