Majani ya malenge ni mboga inayoliwa tumiwa zaidi kutayarisha milo kadhaa. Ni rahisi kukuza na kushughulikia kwani hustawi kwenye aina nyingi za udongo. Malenge huhitajika sana.
Malenge huathiriwa na wadudu kadhaa kama vile panzi, dumuzi, utiriri. Magonjwa ni pamoja na madoa meupe na batobato. Malenge huota baada ya wiki 2 na huwa tayari kuvunwa baada ya mwezi 1. Uvunaji unaweza kufanyika kila baada ya wiki 2 kwa vile mmea hukua haraka.
Mbinu za kukuza malenge
Anza kwa kuchagua udongo ulio na pH ya 6.5 hadi 7, pamoja na mwanga wa jua wa kutosha kwa ukuaji bora wa mimea. Kisha weka mbolea ya kikaboni wiki 2 kabla ya kupanda, na NPK kwa uwiano wa 15:15:15 mwezi 1 baada ya mbegu kuota.
Mbegu zinapoondolewa kwenye tunda, zioshwe na kuzikausha kwa jua kwa muda wa siku 7 ili kupunguza unyevu na kuhimiza uotaji wa mbegu.
Wakati wa kupanda, simamisha mbegu wima huku sehemu ya mbegu iliyochonga ikielekea udongoni. Mwagilia maji kila siku kwa muda wa wiki 2 ili kuhimiza uotaji. Palilia kila baada ya wiki 2 ili kuzuia ushindani wa maji na virutubisho.
Baada ya kuota, simika kijiti kilicho na urefu wa mita 1–2 karibu na mimea ili kuthibitisha shina la mmea, kuhimiza ukuaji wa haraka na kupunguza mashambulio ya magonjwa.
Pogoa mimea au kata majani 8–10 kutoka juu wiki 3 baada ya kuota ili kuongeza mavuno ya mmea. Uvunaji ufanyike baada ya miezi 1–2.