Ufugaji wa nzi aina ya BSF ni fursa ya biashara yenye faida ya kimapato kwa wakulima kwani unahitaji mtaji na ardhi kidogo.
Nzi wazima huhifadhiwa kwa siku 4–7 kwenye banda ambamo huzaliana na kutaga mayai. Baada ya mchakato asili wa kuzaliana nzi jike hutaga mayai karibu na vyanzo vya chakula. Vyanzo vya chakula vinaweza kuwa matunda yaliyoiva, samadi ya ng‘ombe au nyenzo zozote zilizooza ambazo zina harufu kali. Hata hivyo kituo kinapaswa kugawanywa katika sehemu kuu tatu ambazo ni banda la nzi, chombo cha kulishia na chombo cha kutunzia funza ili kurahisisha usimamizi.
Ujenzi wa banda
Anza mchakato kwa kujenga na kuning‘iniza wavu wa urefu wa mita 1, upana wa mita 1 na kina cha urefu wa mita 1.5 juu ya dari ili kuwapa nzi nafasi ya kutosha kupepea.
Hakikisha kuwa wavu unaelekezea chini ili kupata mwanga wa jua zaidi wakati wa mchana. Kisha weka mbao laini chini ya wavu kwa urefu wa futi 2 kuto ardhini ili mwanga wa jua ufikie mbao moja kwa moja.
Kisha funika uso wa mbao kwa damani ya plastiki na uongeze udongo. Weke mmea juu ili kuwapa nzi hisia ya makazi asili.
Kwa vile nzi hawatagi mayai karibu na vyanzo vya chakula bali kwenye mianya na nyufa, hakikisha unajenga mahali pa kutaga mayai ukitumia mbao za vipimo vya upana wa 25cm kwa 25cm.
Weka vifaa vya kutagia mayai juu ya vyanzo vya chakula ndani ya wavu ili kuvutia nzi kutaga mayai ndani.