Soya ni moja wapo ya kunde zinazolimwa na wakulima. Soya ina manufaa kadhaa kwa kuwa ni chakula cha watu, pamoja na chanzo cha protini katika chakula cha wanyama.
Mavuno ya soya ya wastani yanayopatikana kaskazini mwa Ghana ni kati ya kilo 500 hadi 800 kwa hekta, na hii ni chini sana. Kupunguza hasara baada ya kuvuna, uhifadhi bora na kupanda mbegu zilizoboreshwa kunaweza kusaidia wakulima kuongeza mavuno yao. Kwa kupanda aina za mbegu zilizoboreshwa, mavuno yameongezeka hadi kilo 2000 kwa hekta.
Faida za kupanda kwa matuta/ mitaro
Wakulima wanashauriwa kupanda kwenye matuta ili kuimarisha ukuaji wa mimea. Kupanda mimea kwenye matuta ni bora kuliko kupanda kwenye ardhi tambarare kwa sababu ya mvua usiotabirika. Baadhi ya wakati, mvua hunyesha na husababisha mafuriko ndani ya muda mfupi. Wakati wa mafuriko, maji yaliyo kwenye matuta huelekea kwenye mifereji na hivyo huacha matuta hayajafurika.
Kupanda kwenye matuta huhimiza uotaji mzuri wa mbegu, kwani kuingiza kwa maji mengi kunaweza kuzuia uotaji wa soya.
Kupanda kwenye matuta pia huboresha muachano kati ya mimea kwa kuwa matuta huwa yana muachano sawa.