»Kukuza vitunguu nchini Uganda«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=9afHVv6Ovok&t=149s

Muda: 

00:15:10
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

FARM MATTERS

Maarifa juu ya ukuzaji wa vitunguu na mbinu bora za usimamizi ni muhimu katika kuongeza mavuno.

Ukuzaji wa vitunguu huanzia kwenye kitalu. Ili kutengeneza kitalu cha vitunguu, unahitaji udongo mweusi ambao ni tifutifu. Weka mboji na kuichanganya na udongo vizuri. Mboji lazima iwe imeoza kikamilifu kwa sababu mboji mbichi huchoma mbegu za vitunguu. Tawanya mbegu kwenye kitalu na ukitandaze kwa wiki moja. Baada ya wiki moja, ondo nyasi na umwagilie maji mara kwa mara. Miche ya vitunguu huwa tayari kupandikizwa wiki 4 hadi 6 baada ya kupanda

Kupandikiza na kushughulikia mimea

Wakati wa kupandikiza, panda vitunguu kwa muachano wa 10cm kati ya mimea. Vitunguu huchukua takriban miezi 4 kukomaa, lakini wiki 3 za mwisho kabla ya kuvuna huhitaji hali ya hewa isiyo na mvua.

Wadudu waharibifu wa vitunguu ni wadudu chawa, ambao ni hatari sana wakati wa kiangazi kwa sababu hutaga mayai kwenye udongo uliokauka. Umwagiliaji wa maji unaweza kupunguza asilimia kubwa ya mayai hayi. Wadudu chawa wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia kemikali, lakini unyunyizaji wa dawa bora ufanywe jioni.

Ubwiri unga ni ugonjwa hatari wa vitunguu. Unaweza kudhibitiwa kwa kutumia viuatilifu. Tumia dawa za kuzuia ukungu kabla ya ugonjwa kuibuka, pamoja na dawa za kutibu wakati ugonjwa umeshambulia mimea.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:06Katika kitalu, mwagilia miche maji ya kutosha ili kuepusha uharibifu wa miche.
01:0701:14Pandikiza miche ikiwa katika hatua ya majani 4.
01:1502:34Mchakato wa kutengeneza kitalu cha vitunguu.
02:3503:05Dhibiti ukungu kwenye kitalu kwa kutumia kemikali na pia palilia.
03:0605:48Muachanokutoka kwa mmea mmoja hadi mwingine ni 10cm.
05:4908:29Vitunguu huchukua takriban miezi 4 kukomaa, lakini wiki 3 za mwisho kabla ya kuvuna huhitaji hali ya hewa isiyo na mvua.
08:3009:01Wadudu waharibifu wa vitunguu ni wadudu chawa, ambao ni hatari sana wakati wa kiangazi
09:0209:16Wadudu chawa wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia kemikali, lakini unyunyizaji wa dawa bora ufanywe jioni.
09:1710:12Ubwiri unga hushambulia vitunguu vikiwa vichanga na hata vikiwa vimekomaa. Hudhibitiwa kwa kutumia viuatilifu.
10:1315:00Weka vitunguu kwenye masanduku yakaratasi na uvihifadhi mahali pa kavu kwa ajili ya kuvupeleka sokoni.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *