»Jinsi ya kutumia sehemu za juu za miwa kutengeneza silaji«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=_GbeUG4BM30

Muda: 

00:08:01
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Hamiisi Semanda

Miwa ni moja wapo ya zao linalozalishwa na wakulima kwa kiwango kikubwa hasa katika maeneo ya viwanda vya sukari.

Wakati wa uvunaji wa miwa kwa ajili ya usindikaji au ulaji, sehemu za juu za miwa kwa kawaida hukatwa na kutupwa kama taka. Sehemu za juu za miwa zina wanga (sukari) ambayo ni muhimu katika kujenga misuli ya wanyama. Katika mfumo wa kunenepesha, wanyama huwekwa pamoja na kulishwa kwa wingi huku wakipunguza miendo inayosababisha upunguzaji wa nguvu.

Tugengeneza silaji kutoka kwa sehemu za juu za miwa

Ili kutengeneza silage sehemu za juu za miwa hukatwa vipande vidogo kwa kutumia mashine. Vipande vinaweza kuchanganywa na molasi au kushinikizwa ndani ya mifuko ya plastiki.

Mifuko ya plastiki hufungwa, na kisha hufunikwa na udongo.

Hata ukiwa na ardhi ndogo, unaweza kutengeneza silaji. Ukiwa na mashine, unaweza kukata na kutumia mmea wowote kulisha wanyama iwapo hauna sumu.

Baada ya kuchachusha vipande vya juu vya miwa, unaweza kuviondoa kutoka kwenye mfuko wa plastiki na kuwalisha wanyama wako, na vile vile wanyama wanavipenda kwa sababu ya ladha nzuri.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:45Wakati wa uvunaji wa miwa kwa ajili ya usindikaji au ulaji, sehemu za juu ya miwa kwa kawaida hukatwa na kutupwa kama taka
00:4601:40Sehemu za juu za miwa zina wanga (sukari) ambayo ni muhimu katika kujenga misuli ya wanyama
01:4101:52Katika mfumo wa kunenepesha, wanyama huwekwa pamoja na kulishwa kwa wingi huku wakipunguza miendo yao.
01:5302:32Ili kutengeneza silage sehemu za juu za miwa hukatwa vipande vidogo kwa kutumia mashine.
02:3303:30Vipande hushinikizwa kwenye mifuko ya plastiki na kufunikwa na udongo.
03:3105:36Hata ukiwa na ardhi ndogo, unaweza kutengeneza silaji.
05:3706:35Wanyama hupenda sana silaji kutoka kwa vipande vya juu vya miwa kwa sababu.
06:3608:01Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *