Miwa ni moja wapo ya zao linalozalishwa na wakulima kwa kiwango kikubwa hasa katika maeneo ya viwanda vya sukari.
Wakati wa uvunaji wa miwa kwa ajili ya usindikaji au ulaji, sehemu za juu za miwa kwa kawaida hukatwa na kutupwa kama taka. Sehemu za juu za miwa zina wanga (sukari) ambayo ni muhimu katika kujenga misuli ya wanyama. Katika mfumo wa kunenepesha, wanyama huwekwa pamoja na kulishwa kwa wingi huku wakipunguza miendo inayosababisha upunguzaji wa nguvu.
Tugengeneza silaji kutoka kwa sehemu za juu za miwa
Ili kutengeneza silage sehemu za juu za miwa hukatwa vipande vidogo kwa kutumia mashine. Vipande vinaweza kuchanganywa na molasi au kushinikizwa ndani ya mifuko ya plastiki.
Mifuko ya plastiki hufungwa, na kisha hufunikwa na udongo.
Hata ukiwa na ardhi ndogo, unaweza kutengeneza silaji. Ukiwa na mashine, unaweza kukata na kutumia mmea wowote kulisha wanyama iwapo hauna sumu.
Baada ya kuchachusha vipande vya juu vya miwa, unaweza kuviondoa kutoka kwenye mfuko wa plastiki na kuwalisha wanyama wako, na vile vile wanyama wanavipenda kwa sababu ya ladha nzuri.