»sababu 9 za ajabu kwa nini unapaswa kuanzisha ufugaji wa kuku kibiashara«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=uUnZxrWniBQ&t=107s

Muda: 

00:09:13
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Adams Farm Foods

Ufugaji wa kuku ni biashara yenye faida endapo ndege watasimamiwa vyema.

Ndege huathiriwa na tabia mbaya kama vile kujidonoa manyoya na vidole vya miguu. Haya lazima yadhibitiwe ili kuhakikisha ukuaji mzuri wa ndege. Tolea ndege maji safi, kusanya mayai kwa wakati na safisha banda kila wakati ili kuboresha ukuaji wa jumla.

Faida za kuku

Kwanza, mayai ya kuku na nyama huhitajika sana na hivyo kuongeza mapato.

Pia kuku hutoa faida ya haraka, kwani wafugaji wa kuku wa mayai huanza kupata bidhaa kati ya wiki 17– 21, huku wafugaji wa kuku wa nyama wakipata bidhaa kati ya wiki 6–8.

Kuku huhitaji gharama nafuu za uzalishaji kwa vile hawahitaji matumizi ya mashine nzito, na kuku pia wanahitaji nafasi ndogo.

Kuku wa nyama hutoa nyama kwa muda mfupi, na hivyo huleta kipato katika muda mfupi.

Kuku pia hutoa mbolea, hii hutumika kukuza mazao pamoja na kuuzwa.

Kuku huleta utoshelevu wa shamba, kwa sababu ya faida kubwa inayotokana na ufugaji wa kuku. Hatimaye, manyoya ya kuku yanaweza kuuzwa.

Mambo ya kuzingatia

Lisha ndege kwa chakula kilichosawazishwa kwa ukuaji bora na uzalishaji bora wa nyama na mayai.

Jenga mabanda mazuri ili kuboresha afya ya kuku kwa ujumla, na pia punguza midomo ya ndege ili kuepuka kujikula.

Epuka kuweka idadi kubwa ya ndege katika banda moja ili kurahisisha mzunguko wa hewa bila. Geuza matandikoa mara kwa mara ili kuzuia magonjwa.

Hatimaye, anzisha chanzo endelevu cha maji ili kupunguza gharama.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:29Ufugaji wa kuku ni biashara yenye faida endapo ndege watasimamiwa vyema.
01:3001:55Ufugaji wa kuku hutolea wakulima kipato kwa kuuza nyama na mayai
01:5603:05Mayai ya kuku na nyama huhitajika sana na hivyo kuongeza mapato.
03:0604:10Kuku huhitaji gharama nafuu za uzalishaji.
04:1104:52Kuku wa nyama hutoa nyama kwa muda mfupi, na mbolea.
04:5305:51Kuku huleta utoshelevu wa shamba. manyoya ya kuku yanaweza kuuzwa.
05:5206:12Mambo ya kuzingatia kwa ufugaji wa kuku wenye mafanikio.
06:1307:19Lisha ndege kwa chakula kilichosawazishwa kwa ukuaji bora.
07:2007:54Jenga mabanda mazuri ili kuboresha afya ya kuku kwa ujumla
07:5508:25Epuka kuweka idadi kubwa ya ndege katika banda moja
08:2609:13Anzisha chanzo endelevu cha maji ili kupunguza gharama.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *