Bata wanaweza kufugwa bila maji kwa kuwaweka ndani ya banda. Hata hivyo, ukiwafuga bila maji watataga mayai ambayo hayajarutubishwa maana yake hawawezi kuangua mayai. Kwa hivyo, bata dume na maji ni muhimu katika ufugaji.
Vifaranga huhitaji joto hadi watakapokuwa na manyoya kabisa, hivyo joto katika wiki ya kwanza linapaswa kuwa nyuzijoto 90 Selsiasi, na kila wiki baada ya hapo punguza nyuzijoto tano.
Aina za bata
Bata aina ya pekin ni maarufu sana kwa uzalishaji wa nyama kutokana na kiwango chake cha ukuaji wa juu na kufikia kilo 2.5 katika wiki 7–8. Pia ni hutoa faida mbili kwa vile wanaweza kutaga mayai. Bata aina ya muscovy ni maarufu kwa sababu ya hali ya juu ya kuzoea mazingira na uwezo wake wa kujitafutia chakula. Nyama yake ni ladha, lakini hukua polepole.
Kwa uzalishaji wa mayai zingatia aina ya khaki campbell kwani ina uwezo wa kutaga mayai 300–330 kwa mwaka au mayai 175–225 kutegemea aina ya usimamizi.
Masharti ya makazi
Kwa mfumo wa kufugia bata katika banda, mtolee kila bata nafasi ya futi za mraba 4–5 kwa ngege wa mayai, na futi 3 za mraba kwa ndege ya nyama. Kwa mifumo kufugia bata ndani na nje, banda linapaswa kuwa na ufikiaji rahisi.
Tolea kila bata futi za mraba 3–4 kwa makazi ya usiku, na futi za mraba 10–15 kwa bata wanaofugwa huria.
Faida za bata
Wanaweza kuhifadhiwa katika mabanda ya bei nafuu, huchukuwa muda mfupi wa kuzaa, ni sugu kwa magonjwa ya kawaida, na kwa hivyo wana kiwango kidogo cha vifo.