Maji ni rasilimali adimu na mtu anahitaji kuwa na mbinu bora ya kimfumo ya kusimamia maji kwa ukuaji bora wa mazao shambani.
Kwa matumizi bora ya maji, inabidi kwanza kutathmini kiasi cha maji kinachopatikana kisha kujua jinsi ya kuyatumia kwa ufanisi katika uzalishaji wa mazao. Maji yakiwa mengi kwenye udongo ndivyo hewa inavyopungua kwenye udongo. Vyanzo mbalimbali vya maji ni pamoja na maji ya mito, maji ya mvua, maji ya visima na maji yanayotiririka kwenye mabwawa.
Mbinu za umwagiliaji
Unapopanga kutumia maji, unapaswa kuzingatia njia utakayotumia na kiasi cha maji kinachopatikana. Umwagiliaji kwa njia ya matone ina ufanisi zaidi hata hivyo, ni bei ghali.
Umwagiliaji kwa njia ya mifereji huhitaji maji mengi, na husababisha mmomonyoko wa udongo, utuamaji wa maji na uvujaji wa virutubisho. Uvujaji wa udongo ni upotevu wa virutubisho huku vikiingia sehemu ya ardhi ya chini.
Ufuatiliaji
Ufuatiliaji husaidia mtu kujua ni kiasi gani cha maji kinachoingia kwenye mazao, kwa kiwango gani na muda gani maji yatahitajika kwa mazao. Kutathmini mmea husaidia kukidiria kama mmea unahitaji maji zaidi au laa.
Unaweza pia kutathmini kiwango cha maji kwenye udongo kwa kufinya udongo kati ya kiganja ili kutengeneza mpira. Dondosha mpira chini na ikiwa mpira hutavunjika, udongo una maji ya kutosha. Ikiwa mpira utavunjika, inamaanisha kuwa maji hayatoshi kwa ukuaji wa mazao.
Changamoto za kusukuma maji
Kusukuma maji ni ghali katika suala la matumizi ya umeme.
Pia husababisha uvujaji wa virutubisho.
Faida za kutumia maji
Kutumia rasilimali ya maji kwa busara huhakikisha kwamba mazao yanadumishwa kwa muda mrefu. Pia huboresha mavuno ya mazao, na hivyo kuhakikisha kwamba wakulima wanapata faida nzuri.