Kupukuchua na kupura ni mojawapo ya hatua zinazoboresha thamani ya soko la mahindi na kupunguza hasara ya baada ya mavuno kwenye mnyororo wa thamani wa mahindi.
Kupukuchua hufanywa baada ya kuvuna, kwa hivyo kujifunza mchakato huo ni muhimu sana kwa wakulima wa mahindi. Kutumia mtambo kupura ni bora kuliko kutima mikono kwani muda mfupi unatumika katika kusafisha na kupepeta mahindi. vinginevyo upuraji kwa mikono unaweza pia kutumiwa na wakulima wenye uwezo mdogo wa kupata mitambo. Hata hivyo huku kufanyike kwa uangalifu ili kuepuka kuvunja punje za mahindi kwani punje zilizovunjwa hushambuliwa sana na wadudu, na hivyo kusababisha bei duni ya mahindi sokoni.
Hatua za kufuatwa
Mwanzoni mwa mchakato, sogeza gunzi za mahindi kwenye kivuli ili kujikinga dhidi ya jua kwa kuwa kupukuchua huchukua muda mwingi. kisha fungua sehemu ya juu ya gunzi kwa kutumia kitu chenye ncha kali na uondoe maganda. Kisha tenganisha punje gunzi ili kudumisha ubora. Walakini, upuraji kwa mtambo ni muhimu sana kwani husababisha uharibifu mdogo kwa nafaka na ni haraka.
Wakati wa uvunaji wa mitambo ni muhimu sana kurekebisha ukubwa wa sehemu ya mtambo ya kupuria ukilinganishwa na ukubwa wa nafaka ili kuepuka kuvunja nafaka au kuacha nafaka kwenye gunzi la mahindi. Kusanya nafaka zilizomwagika ili kuepuka hasara baada ya mavuno.