Kugeuza asali kuwa pesa

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/turning-honey-money-0

Muda: 

11:00:00
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Access Agriculture

Uuzaji wa bidhaa

Nyuki hukusanya maji matamu kutoka kwa maua katika msimu wa mvua ili kutengeneza asali ambayo hukomaa katika miezi 2-3 baada ya mvua kuanza. Mkulima anapaswa kuvuna asali ambayo imekomaa kwa ubora tu. Jua linapotua, nyuki huwa na shughuli kidogo na hawawezi kuuma.Jua linapotua, kwa hivyo mkulima anapaswa kuvaa vifaa vya kujikinga anapokuvuna asali.
Vile vile, safisha na kausha vifaa vya kuvunia na kusindika asali. Vuna tu masega yaliyofungwa na ambayo hayajaharibika kwa vile haya huwa yana asali iliyokomaa ambayo pia inawezakuhifadhiwa kwa muda mrefu. Epuka kuvuna masega ambayo hayajafungwa. Anza usindikaji mara baada ya kuvuna masega kwa kuondoa nyuki juu ya masega, na kuweka masega kwenye ndoo. Pia tenganisha sehemu za masega ambayo hayajafungwa kwani haya yana asali ambayo haijakomaa yenye maji mengi ambayo huharibu asali haraka.
Weka kipande cha masega ambayo hayajafungwa kwenye ndoo nyingine na ondoa masega yenye chavua nyingi kwani haya hupunguza ubora na thamani ya asali. Chimba asali kwa kusafisha na kuponda masega. Weka masega yaliyopondwa kwenye ndoo iliyotobolewa matundu na kuininginiza juu ya ndoo kubwa zaidi ili kuchuja asali.
Zaidi ya hayo, funika ndoo na mfuko mweusi wa plastiki ili joto lisitokee. Weka ndoo kwenye jua moja kwa moja angalau saa 3 kutegemeana na wingi wa asali utakayochakata, pamoja na kiwango cha jua. Kisha chukua vyombo ndani ili kuchuja zaidi na pakia asali mara baada ya kuchuja kwani asali inaweza kunyonya maji ikiachwa wazi, na hivyo kuharibika haraka.
Pakia asali kwenye glasi au chupa za pastiki na kuihifadhi vizuri au kuiza.
Hatimaye, toa nta kutoka kwenye masega yaliyotumika, haya huwa dhabiti baada ya saa 24 na huelea juu ya maji.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:29Bidhaa za nyuki zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko bidhaa zingine
00:3001:50Asali ni chakula cha asili chenye faida nyingi za kiafya.
01:5102:11Asali iliyosindikwa inaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
02:1202:26Kwa ubora, vuna asali iliyokomaa tu.
02:2702:32Dumisha usafi wakati wa kuvuna na kusindika
02:3302:41Daima hakikisha vifaa viko safi.
02:4202:53Nyuki hukusanya maji matamu kutoka kwa maua katika msimu wa mvua
02:5403:00Asali hukomaa katika miezi 2-3 baada ya mvua kuanza
03:0103:16 Jua linapotua, nyuki huwa na shughuli kidogo na hawawezi kuuma.
03:1703:25kuvaa vifaa vya kujikinga anapokuvuna asali.
03:2603:58 safisha na kausha vifaa vya kuvunia na kusindika asali
03:5904:13Vuna tu masega yaliyofungwa na ambayo hayajaharibika
04:1404:20Epuka kuvuna masega ambayo hayajafungwa
04:2104:45Anza usindikaji mara baada ya kuvuna masega
04:4604:55Ondoa nyuki juu ya masega, na weka masega kwenye ndoo
04:5605:06 tenganisha sehemu za masega ambayo hayajafungwa
05:0705:11Weka kipande cha masega ambayo hayajafungwa kwenye ndoo nyingine
05:1205:22ondoa masega yenye chavua nyingi
05:2305:49Chimba asali kwa kusafisha na kuponda masega
05:5005:59Weka masega yaliyopondwa kwenye ndoo iliyotobolewa matundu na kuininginiza juu ya ndoo kubwa zaidi ili kuchuja asali.
06:0006:07funika ndoo na mfuko mweusi wa plastiki ili joto lisitokee.
06:0806:27 Weka ndoo kwenye jua moja kwa moja angalau saa 3
06:2807:00chukua vyombo ndani ili kuchuja zaidi
07:0107:40 pakia asali mara baada ya kuchuja
07:4108:28Pakia asali kwenye glasi au chupa za pastiki
08:2908:50Pakia asali kwenye glasi au chupa za pastiki na kuihifadhi vizuri au kuiza.
08:5109:47toa nta kutoka kwenye masega yaliyotumika
09:4811:00muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi