Kabla ya kupanda mti wa tende, hakikisha kwamba unaupanda katika eneo ambalo mti unapata mwanga wa jua moja kwa moja, na mahali pana ili mti ukue vya kutosha.
Mazinagtio wakati wa kupanda
Chimba shimo la kupandia lenye kina cha futi 3 na kipenyo cha futi 3 mahali pasipotwamisha maji. Ili kujua hilo, mimina maji kwenye shimo na ikiwa hayatapenya ardhini ndani ya masaa 24, jua kwamba udongo si uzuri.
Chimba shimo ambalo ni kubwa kuliko kiriba kilicho na mmea.
Wakati wa kuchimba shimo, tenganisha udongo wa juu kutoka kwa udongo wa chini.
Changanya udongo wa juu na mboji kwani hii ndiyo itakayotumika kujaza shimo baada ya kupanda.
Kupanda miche
Anza kwa kujaza tena udongo uliochanganywa na mboji.
Usipande miche kwa kina kirefu.
Ondoa mche kutoka kwa kiriba au chombo.
Ingiza mche kwenye shimo na ujaze shimo kwa udongo wa juu uliobaki uliochanganywa na mboji.
Ongeza mboji kuzunguka mche na kisha mwagilia maji.