»Dondoo ya kiini cha mbegu za mwarobaini«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/neem-seed-kernel-extract

Muda: 

00:15:11
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Atul Pagar, WOTR

Kutumia viuatilifu vya kemikali ni ghali, na ni hatari kwa watu na mazingira. Viuatilifu huua wadudu wenye manufaa ambao hula na kuua wadudu waharibifu. Viuatilifu pia huathiri udongo na maji.

Dawa asili zina vyanzo vya asili ambavyo vinadhibiti wadudu waharibifu, na ni rahisi kutumia, ni bei nafuu, na haziachi mabaki kwenye mimea. Dawa hizi zinafaa kutumiwa tu wakati zinahitajika na kwenye mimea iliyovamiwa na wadudu.

Faida za dawa asili

Majani ya mwarobaini yana dawa za asili ambazo hufanya mimea kuwa na ladha mbaya na hivyo huzuia mimea kuliwa na wadudu kama vile vidukari, nzi weupe na vipeperushi wa mimea.

Mimea hufyonza dondoo ya mwarobaini kupitia majani na mizizi na hivyo kuwadhibiti dumuzi ambao hula matawi ya ndani na mara nyingi hawaathiriwi na dawa ambazo hufikia tu sehemu ya nje ya mmea.

Dawa asili haziathiri wadudu wenye manufaa, wala mazingira kwani huoza kiasili.

Jinsi ya kuandaa dondoa

Kusanya matunda ya mwarobaini yaliyoiva kabisa ambayo yana rangi ya manjano au yale ya hudhurungi yaliyoanguka chini.

Loweka matunda ya mwarobaini kwenye maji kwa masaa 24 na uondoe maganda. Tandaza mbegu kwenye mkeka hadi zitakapokauka. Maganda yanaweza kutumika kwenye mbolea.

Matumizi ya dondoo la mwarobaini

Ili kuandaa dodoo ya kiini cha mbegu za mwarobaini, saga 5 kgs za mbegu hadi ziwe unga huku ukifunika pua yako kuzuia kichefuchefu au kutapika. Changanya unga kwa lita 10 za maji. Kwa ufanisi mzuri, ongeza vijiko 20 vya unga wa sabuni asili ili kuwezesha mchanganyiko kunata kwa mimea.

Weka mchanganyiko kwenye kivuli kwa masaa 24. Baada ya masaa 24 koroga mchanganyiko na uchuje mara 2 hadi 3. Tumia kitambaa cha pamba iwapo unachuja ili kuzuia chembechembe kuziba ncha ya bomba la dawa.

Nyunyiza mchanganyiko kabla ya mmea kutoa maua au wakati maganda yanatengenezwa. Athari zinaweza kuonekana baada ya siku 7 hadi 10. Katika msimu wa mvua, nyunyiza mchanganyiko mara nyingi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:10Kutumia viuatilifu vya kemikali ni ghali, na ni hatari kwa watu na mazingira na huua wadudu wazuri.
01:1102:17Dawa asili zina vyanzo vya asili ambavyo vinadhibiti wadudu waharibifu,
02:1803:08Majani ya mwarobaini yana dawa za asili ambayo huzuia mimea kuliwa na wadudu.
03:0904:05Mimea hufyonza dondoo ya mwarobaini kupitia majani na mizizi
04:0604:48Dondoo la mwarobaini si hatari kwa mazingira, na hudhibiti wadudu kama vile vidukari, nzi weupe na vipeperushi wa mimea
04:4905:40Tumia matunda ya mwarobaini yaliyoiva kabisa ambayo yana rangi ya manjano au yale ya hudhurungi kuandaa dondoo
05:4106:25Loweka matunda ya mwarobaini kwenye maji na ondoa maganda. Maganda yanaweza kutumika kwenye mbolea
06:2607:40Hifadhi mbegu zilizokaushwa kwenye magunia. Saga mbegu za mwarobaini huku ukifunika pua yako kwa barakoa
07:4108:20Epuka kutumia vyombo vya chuma kwa sababu vinashika kutu kwa urahisi
08:2110:25Ongeza unga wa sabuni asili kwenye mchanganyiko. Weka mchanganyiko kwenye kivuli kwa masaa 24 na kisha ukoroge. Tumia kitambaa cha pamba iwapo unachuja.
10:2613:00Safisha ncha ya bomba la dawa. Nyunyiza mchanganyiko kabla ya mmea kutoa maua au wakati maganda yatakapoanza kutengenezwa
13:0115:11Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *