Ni muhimu kuchukua tahadhari wakati wa kusafirisha mifuko ya mbegu au nafaka kwa sababu nyenzo zenye ncha kali zinaweza kurarua mifuko yako na kusababisha hasara kwa mazao.
Kabla ya kuanza kupakia mazao kwa ajili ya usafirishaji, safisha lori ili kuondoa mabaki ya awali, ziba mashimo kwenye sakafu au paa na pakia mifuko kwa usawa, walakin epuka kupakia zaidi kupita kiasa.
Baada ya kupakia, funika mifuko ili kuepuka kuchafuliwa na ndege au mvua lakini wakati wa kufunika, weka vipande vilivyopinda vilivyotengenezwa kwa mianzi au chuma ili kuzuia mkusanyiko wa maji juu ya turubai. Kisha funika sehemu ya juu na upanue turubai kutoka juu ili iweze kufunika pande zote za lori, na funga vizuri.
Wakati wa kusafirisha, fanya vituo vya mara kwa mara unaposafiri na uangalie hali ya mizigo na ikiwa ni lazima, panga upya mzigo.