Kukuza uyoga ni rahisi na hufanya kama chanzo mbadala cha mapato. Uyoga unaokuzwa kawaida ni uyoga chaza.
Uyoga chaza hupendelewa kwa vile ni ladha, ni rahisi kukuzwa, hukua haraka, na hukua kwenye aina mbalimbali za msingi au nyenzo. Kilimo cha uyoga ni biashara yenye faida kwani inahitaji mtaji mdogo, nafasi ndogo, ni chanzo cha mapato na pia uyoga huzaa mara mbili kila baada ya saa 24. Hata hivyo, kilimo cha uyoga kinahitaji usafi. Uyoga unaweza kupandwa kwenye mifuko ya plastiki au ndoo yenye mashimo.
Hatua za kufuata
Kwanza, tayarisha msingi kutoka kwa nyenzo zinazopatikana kwa urahisi kama vile maganda ya karanga, gunzi za mahindi, ushwa wa mahindi na ngano, maganda ya mahindi, pumba za mpunga, makapi ya pamba, taka za mbao, majani ya migomba, na nyasi kavu.
Kisha jaza maji kwenye chombo cha plastiki, na kwa kila lita 100 za maji weka gram 50–75 ya chokaa ili kuua vijidudu na viini.
Kata nyenzo katika vipande vidogo na uviloweke kikamilifu kwenye maji yaliyochanganya na chokaa ndani ya pipa.
Osha mikono vizuri kwa sabuni na pia tumia dawa ya kuua vijidudu.
Kisha ondoa maji kutoka kwenye nyenzo kwa kuzifinya kwa mikono na utandaze nyezo kwenye mfuko wa plastiki au ndoo na kisha tandanza mbegu juu ya nyenzo.
Endelea kuongeza tabaka au safu nyingi za nyenzo huku ukiweka mbegu pamoja na kubonyeza kila tabaka. Kisha funga mifuko ya plasiki au funga kifuniko cha ndoo, na kisha toboa mifuko ya plasiki ukitumia kisu safi ili kuingiza hewa ya oksijeni kwenye msingi au nyenzo.
Weka misingi ya uyoga (mifuko ya plasiki) chumbani kilicho na giza pamoja na halijoto la 20–24C ili kuwezesha mbegu kuota na kuanza kukua.
Anza kumwagilia maji mara 2–3 kwa siku wakati uyoga kuzaa. Toboa mashimo mengine kwenye mifuko ya plastiki ili kuwezesha uyoga zaidi kuibuka.
Mwishowe, endelea kumwagilia maji kwa siku 7 zijazo na uvune wakati umbo la mwavuli linaanza kutoweka.