Muhogo ni moja wapo ya mazao makuu yanayolimwa barani Afrika. Mbinu sahihi kabla, wakati wa na baada ya kupanda husaidia kuongeza mavuno.
Kabla ya kupanda muhogo, hakikisha una eneo zuri la kulimia muhogo. Kwa mavuno mazuri, unahitaji udongo tifutifu au wa kichanga. Eneo lisiwe na maji mengi sana, lisiwe na kina kifupu wala na mwinuko. Chunguza eneo kwa uangalifu na utambue magugu yalipo kama vile nyasi, majani, magugu ya kudumu au ya kila mwaka kwa sababu haya yanaweza kuathiri mazao.
Shughuli za shambani
Kabla ya kupanda, hakikisha kuwa umetayarisha ardhi yako vizuri. Kwa hivyo, unaweza kuamua kutengeneza matuta au la.
Mashina yanapaswa kukatwa katika vipande vya urefu wa 25cm, na panda wakati udongo una unyevu wa kutosha.
Muachano kati ya mihogo hutegemea kusudi la kupanda muhogo. Ikiwa mihogo inapandwa kwa ajili ya uzalishaji wa mashina au vipandwa basi, panda kwa umbali wa 1m kati ya mistari na 0.5m kati ya mimea. Iwapo mihogo inapandwa kwa ajili ya mizizi, acha umbali wa 1m kwa 0.8m.
Weka dawa ya kuua magugu ndani ya saa 24 baada ya kupanda ili kuchelewesha uotaji wa magugu.
Baada ya wiki 2–3, jaza pengo kwenye mahali ambapo mmea haukuota ili kuhakikisha kuwa una idadi ya mimea inayofaa. Hii ni bora kufanywa kwa wakati sahihi kwa sababu ukichelewa, mimea iliyokua itazuia upenyaji wa mwanga wa jua kwa mimea michanga.